Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 5, 2013

KINANA AWAKONGA MOYO WAKAZI WA MBEYA.


Katibu wa Itikadi na Uenezi  CCM Taifa, Nape Nnauye akiwahutubia maelfu wa Wananchi wa Jiji la Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi RuandaNzovwe.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akisalimiana na Nape katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mbeya waliofurika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika viwanja vya shule ya Msingi RuandaNzovwe Jijini Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akijibu baadhi ya kero za Wananchi katika mkutano huo.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amepozi baada ya kuvalishwa mavazi ya kichifu na wazee wa mila wa Mkoa wa Mbeya ambavyo ni Mkuki, mgolole na kigoda.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi wa Jiji la Mbeya katika Mkutano huo.

Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa Mkoa wa Mbeya kupitia UVCCM, Nwaka Mwakisu akiwa amebebwa juu kwa juu na vijana kwa mchango wake mkubwa kwa vijana wa Mbeya

Meza kuu wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio yanayoendelea jukwaani.

Vijana wa Mwanjelwa wakiwa wamembeba msombesombe mlezi wao Mbunge wa Viti maalum Mary Mwanjelwa wakimpeleka kwenye gari lake baada ya kukamilika kwa mkutano.
PICHA NA MBEYA YETU BLOG.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana, ameonesha kukubalika kwa wananchi na Wakazi wa Jiji la Mbeya baada ya yeye na ujumbe wake kupata mapokezi makubwa tofauti na matarajio ya watu wengi kutokana na Jiji la Mbeya kuongozwa na Mbunge wa Chadema.

Kinana aliyekuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vya jirani katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ruandanzovwe Ilomba Jijini Mbeya, aliwakonga watu waliofurika uwanjani hapo kutokana na kile alichokuwa akiwahutubia kuwagusa hadi moyoni.

Kinana huku akishangiliwa na umati wa wananchi bila kujali itikadi zao alisema Chama cha Mapinduzi hakina sababu ya kujiita Nambariwani kutokana na kuwakandamiza wananchi wa hali ya chini na kuishi maisha magumu kutokana na viongozi wa chama hicho ngazi ya juu kufanya ndivyo sivyo.

Alisema Chama cha Mapinduzi ndicho chenye Serikali hivyo kitendo cha kuuza viwanda kwa Wawekezaji ambao wameshindwa kuviendeleza ni kuwakosesha fursa wananchi ya kufaidi matunda ya nchi yao ambapo aliongeza kuwa kama Serikali iliona watu hao walishindwa kuviendeleza viwanda hivyo ni bora wakapokonywa wakapewa watu wengine wanaweza kufanya kazi ili watanzania wengi wapate ajira.

Aliongeza kuwa Katiba ya Nchi inasema hakuna mtu aliyejuu ya mwingine zaidi ya Wananchi, hivyo viongozi wa Serikali hususani Mawaziri hawana sababu ya kuwapangia wananchi kitu cha kufanya bali wanatakiwa kuwauliza wanachotaka kufanyiwa ni nini kwa sababu wananchi ndiyo wako juu ya viongozi.

Katika Mkutano huo Kinana alisimikwa kuwa Mkazi wa Mbeya baada ya kuvalishwa Mgolole na kupewa Mkuki na kigoda na viongozi wa kimila wa Mkoa wa Mbeya kama ishara ya kumkaribisha Mkoani hapa.

Wakati Mkutano ukimalizika uwanjani hapo baadhi ya Vijana wa Mwanjelwa ambao walitaka kujiunga na chama cha mapinduzi na kuomba kukabidhiwa kadi za chama hicho ambapo jukumu la kuwakabidhi aliachiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa (Mnec) Capt. Shitambala, waliwasifia walezi wao kwa kuwaunganisha na chama pamoja na misaada mbali mbali.

Vijana hao walipotakiwa kusema lolote mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye, walisema juhudi za wao kuonekana na kusimama mbele ya jukwaa ni kutokana na elimu nzuri waliopewa na walezi wao ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa Mkoa wa Mbeya kupitia UVCCM, Nwaka Mwakisu na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa.

Walisema walezi hao huwasaidia pindi wakiwa na matatizo mbali mbali ya kiushauri na kifedha kwa kuwaunganisha pamoja na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya vyama vya Siasa ambavyo huwatanguliza mbele kwenye vurugu ili hali wao hubaki nyuma na kukimbia.

Na Mbeya yetu
No comments: