WATUHUMIWA wawili kati ya wanne wa
kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Rungwe, John Mwankenja, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na
hatia katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama
kuu kanda ya Mbeya iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya
ya Rungwe chini ya Jaji Samweli Karua, baada ya kuahirishwa kutolewa kwa hukumu
hiyo kwa zaidi ya mara tatu na kuzua hali ya sintofahamu kwa ndugu wa
washtakiwa na wafuatiliaji wa kesi hiyo.
Awali kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo
Mwendesha mashtaka wa Serikali., Archiles Mulisa, aliwataja watuhumiwa wote
wanne kuwa ni Hakimu Mwakalinga, Daudi Mwasipasa, Obote Mwanyingili na Kelvin
Myovela wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa maksudi aliyekuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe John Mwankenja.
Alisema
watuhumiwa hao wenye kesi namba 131/2012 walitenda kosa hilo Mei 19, 2011
katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Mulisa
aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali Lugano Mwakilasa kwa upande wa
mashtaka huku Watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili ambao ni Victor
Mkumbe na Simon Mwakolo.
Mulisa
alidai mahakamani hapo kuwa kesi inayowakabili watuhumiwa hao walilitenda
Mei 19,2011 kwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja kinyume na kifungu cha 196
sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Karua ambaye alianza majira ya saa 14:37 mchana na kukamilisha
saa 15:37 alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka na utetezi haubishaniwi
kuhusu kifo cha marehemu.
Aliongeza
kuwa pande hizo mbili pia hazibishaniwi kuhusu ripoti za kitaalamu na dhamira
za mauaji hayo bali kinachobishaniwa ni uhusika wa watuhumiwa hao dhidi ya
mauaji hayo.
Alisema
katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulileta mashahidi 11 ambao wote kwa
pamoja wakiongozwa na shahidi namba moja waliwatuhumu washtakiwa kuhusika
na tukio hilo.
Shahidi
huyo namba moja Weston Jacob(17) mkazi wa Kiwira Mwanafunzi kidato cha Tatu katika
shule ya Sekondari Kipoke ambaye pia ni Mjomba wa marehemu ambaye aliiambia
mahakama kuwa siku ya tukio akiwa nyumbani akijisomea majira ya 2: 30 usiku
ambapo marehemu alifika nyumbani na kupiga honi ya gari akitaka afunguliwe
mlango.
Mbali
na ushahidi huo Jaji Karua alisema pamoja na ushauri wa wazee wa baraza la
mahakama ambao pia wanawatuhumu washtakiwa hao kuhusika na tukio hilo nae
anakubaliana nao lakini siyo kwa watuhumiwa wote.
Kutokana
na ushahidi huo alisema Mshtakiwa namba moja na namba mbili ambao ni Hakimu
Mwakalinga na Daudi Mwasipasa wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa moja na mauaji
kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua maelezo na vipimo vya
vinasaba.
Alisema
Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye anatiwa hatiani kutokana na kosa la
kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji hivyo yeye
hausiki moja kwa moja na kosa hilo.
Jaji
karua alisema kwa upande wa mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela anatiwa hatiani
kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika nkatika mauaji hayo ingawa hakusika na
kitendo hicho moja kwa moja.
Aliongeza
kuwa kutokana na kifungu cha sheria cha mwenendo wa makosa ya jinai kifungu
namba 300 na 217 washtakiwa namba tatu na namba nne wanatiwa hatiani na
mahakama.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles
Mulisa, aliiambia mahakama hiyo kwamba itoe adhabu kali kutokana na kitendo
alichofanyiwa marehemu na iwe fundisho kwa watu wengine.
Kwa upande wa utetezi ambao siku ya
hukumu uliwakilishwa na Wakili Merick Luvinga alisema mahakama iwanee huruma
washtakiwa kwa kuwa wote umri wao ni mdogo wanaweza kujifunza na kurudi
kuungana na jamii pia ni kosa lao la kwanza hivyo wasipewe adhabu kali.
Kutokana na utetezi huo, Jaji Karua
alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika
pasipo shaka kwa washtakiwa namba moja na namba mbili hivyo adhabu yao ni
kunyongwa hadi kufa.
Aliongeza kuwa Mshtakiwa namba tatu
Obote Mwanyingili anayehusika kumhifadhi mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka
saba kwa kosa hilo sambamba na mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela
aliyehifadhi silaha iliyotumika kwenye mauaji.
Alisema kutokana kosa hilo mtuhumiwa
huyo atatumikia kifungo jela miaka saba ingawa pia tayari alikuwa amehukumiwa
kifungo jela cha miaka 20 kwa kosa la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
Wakati huohuo
MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imemhukumu
kwenda jela miaka 35 mtuhumiwa wa mauaji dhidi ya watoto huku mwingine
akiachiwa huru baada ya kukutwa bila hatia.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa
Mahakama kuu kanda ya Mbeya Samweli Karua mbele ya mwendesha mashtaka wa
serikali Archiles Mulisa katika vikao vilivyofanyika katika Mahakama ya wilaya
ya Rungwe.
Awali mwendesha mashtaka wa serikali
Archiles Mulisa aliiambia mahakama kuwa washtakiwa Baraka Mwandibwa na Zuberi
Lwila walifikishwa mahakamani hapo wa kosa la kumlawiti na kumuua mtoto Esta
James(5) Novemba 21, 2010.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria
kifungu cha 196 (16) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambalo walilifanya
katika kijiji cha Bulyaga Wilayani Rungwe baada ya kumteka mtoto huyo.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua alisema
Mshtakiwa namba moja anatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo ambao ulitoka kwa shahidi namba moja ambaye ni mtoto aliyejulikana kwa
jina la Marietha.
Alisema mtoto huyo ambaye alisema siku
ya tukio alikuwa akicheza na marehemu ambapo mtuhumiwa alifika na kumpa pipi
aina ya Ivory marehemu kisha kuondoka naye ambapo shahidi huyo aliwerza
kumtambua mtuhumiwa katika gwaride la utambuzi.
Mbali na hilo alisema ushahidi mwingine
ni ushaidi wa Vinasaba ambao unawahusisha moja kwa moja watuhumiwa wote wawili
ikiwa ni pamoja na ushaidi wa kimazingira unaomhusisha mtuhumiwa wa kwanza.
Alisema kutokana na ushahidi huo
Mtuhumiwa wa kwanza anahusika moja kwa moja na mahakama inamtia hatiani ingwa
kwa mujibu wa ushahidi hakuua kwa makusudi kutokana na kutokuwa na vifaa vya
mauaji kama visu panga na silaha zingine.
Alisema katika mwili wa marehemu
ulikutwa ukiwa unadamu na mbegu za kiume sehemu zake za siri na hakuwa
amejeruhiwa nsehemu yoyote, hivyo mahakama iliona mtuhumiwa hakuua kwa
kukusudia bali ilikuwa ni bahati mbaya.
Hata hivyo upande wa Mshtaka uliomba
mahakama itoe adhabu kubwa na kali dhidi ya washtakiwa kutokana na mazingira
aliyofanyiwa mtoto huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za
kuwalaghai watoto wadogo.
Akitoa hukumu hiyo Jaji karua alisema anakubaliana
na ushauri wa upande wa mashtaka kwamba tukio hilo ni kubwa na mstakiwa wa
kwanza Baraka Mwandibwa ataenda jela kwa miaka 35 huku mshtakiwa wa pili Zuberi
Lwila akiachiwa huru baada ya kutokuwa na ushahidi wa kuhusika katika tukio
hilo.
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment