Watanzania wametakiwa kubadilika kutoka
kulima kilimo cha mazoea na kujikita katika uzalishaji unaolenga mahitaji ya
soko la nje ili kuboresha vipato na maisha yao kutokana na uwepo wa fursa.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
mtendaji wa taasisi ya TAHA, Jackline Mkindi wakati akizungumza katika Mkutano
wa wadau wa kilimo cha mazao ya mboga mboga, maua na matunda kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la ukaguzi jijini Mbeya.
Mkindi amesema wananchi wengi hawajui
kuwa kilimo hicho ni rahisi na kinaweza kubadilisha maisha yao kwa muda mfupi
tofauti na mazao mengine ambayo yanachukua muda mrefu hadi kuvunwa kwake.
Amesema ni bora wakajikita katika uzalishaji
wa mazao hayo wakilenga mahitaji ya soko la nje kwa kuzingatia uwepo wa fursa
ya uwanja wa kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kusafirisha mazao hayo hadi
Sokoni.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbasi Kandoro aliwataka viongozi wenzie kuacha porojo na kutekeleza Agizo la
Raisi Kikwete kwa vitendo kuhusu kutumia fursa ya Uwanja wa Ndege wa Songwe
katika kilimo cha mazao ya m,atunda, maua na mboga mboga.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa
Mikoa wa Mbeya, Njombe na Iringa pamoja na makatibu tawala, Wakuu wa Wilaya na
wataalamu wa Kilimo cha mazao hayo kutokana na kuwa na mpango wa pamoja katika
kilimo hicho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment