MAONESHO ya kimataifa ya biashara
yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa
Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya yamekamilika kwa asilimia tisini baada ya
makampuni kutoka ndani na nje ya nchi kufika.
Baadhi ya makampuni yaliyojitokeza ni
kutoka Nchini Kenya, ambapo mmoja wa washiriki wa maonesho hayo kutoka nchini
humo aliyejitambulisha kwa jina la Charles amesema wameshafika na wako tayari
kwa maonesho isipokuwa wenzao kama makampuni manne wako njiani.
Makampuni mengine ni kutoka Jijini Mbeya
kama Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Benki ya NMB, Benki ya CBA, Wajasiliamali
mbali mbali kama vile Marmo Granito na wengine wengi ambao tayari
wameshapanga bidhaa zao tayari kwa maonesho.
Hata hivyo maonesho hayo yanatarajiwa
kufunguliwa rasmi kesho na kwa mujibu wa baadhi ya wajumbe wa TCCIA wamesema
mgeni rasmi wa kufungua maonesho hayo ni Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison
Mwakyembe maonesho ambayo yatadumu kwa zaidi ya wiki moja.
Endelea kufuatilia mtandao wetu kwa
taarifa na matukio zaidi ya maonesho hayo……
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment