Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mmoja wa wahanga aliyefahamika kwa jina la Luchina Mgaya(55) mkazi wa kijiji cha Utulo alisema wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu baada ya kupata ulemavu hivyo kushindwa kujitafutia riziki.
FAMILIA moja katika kijiji cha Utulo
wilaya ya Mbarali Mkoani hapa imepata ulemavu wa viungo baada ya kudaiwa
kupigwa na kujeruhiwa na wafugaji jamii ya kisukuma.
Tukio hilo la kusikitisha liliikumba
familia hiyo Januari Mwaka huu baada ya baba, Mama na mtoto kupata ulemavu
baada ya kukosa matibabu yaliyotokana na kukosa msaada wa fedha kutoka kwa
wanaotuhumiwa kutyenda kosa hilo.
Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mmoja
wa wahanga aliyefahamika kwa jina la Luchina Mgaya(55) mkazi wa kijiji cha
Utulo alisema wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu baada ya kupata
ulemavu hivyo kushindwa kujitafutia riziki.
Luchina amesema alipigwa na wafugaji hao
mapema mwaka huu baada ya mwanae wa kiume kuvamiwa na wafugaji hao wakidai kuwa
aliwachongea kwenye uongozi wa kijiji hali iliyopelekea kukamatwa.
Alisema Baada ya kuona mwanae anapigwa
mama huyo alifanya jitihada za kumuokoa ili asipate kipigo ndipo walipomgeukia
na kumpa kipigo kikali yeye na mumewe ambapo yeye amepata ulemavu wa viungo na
mumewe akiwa amepata upofu.
Luchina ametabanaisha kuwa baada ya
kipigo kikali walitoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji na Polisi Rujewa ambapo
watuhumiwa walikamatwa na kufunguliwa kesi lakini wakaomba kesi hiyo waimalize
nje ya mahakama jambo ambalo walikubaliana nalo.
Aliongeza kuwa Pamoja na kukubaliana
suala hilo kulimaliza nje ya mahakama ambapo watuhumiwa walikiri kutenda kosa
na kuahidi kulipa jumla ya shilingi laki tano ikiwa ni gharama za matibabu na
shilingi milioni nne ambazo ni fidia waliahidi kulipa kwa muda wa siku mbili
tu.
Mhanga huyo alisema kitu cha kushangaza
ni kitendo kilichofanywa na watu waliopewa dhamana ya kutunza amani na
sheria ambao ni Mwenyekiti wa kijiji na Askari mpelezi wa kesi hiyo kuzitafuna
pesa hizo na kuwaacha wahanga hawana kitu mpaka leo.
Hata hivyo baadhi ya wanaotuhumiwa
kuwazunguka wahanga hao walipotafutwa kuthibitisha kutenda kosa hilo waligoma
kulizumzia kwa kile walichodai hawalijui kabisa.
Aidha familia ya Luchina imekuwa ikiishi
maisha ya ombaomba, pamoja na kufukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi kwa
kukosa pesa za kulipa pango la nyumba na watoto watatu wameacha masomo
kutokana na kukosa ada.
Wahanga hao wameziomba taasisi
mbalimbali kuwasaidia ili waweze kupata haki zao kwani wamejitahidi kufuatilia
maeneo yote lakini wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tamaa na wao kukata
tama ya kuishi.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya, Diwani Athumani amekili kupata taarifa za tukio hilo na kuahidi
kulifuatilia na kulipatia ufumbuzi ndani ya mfupi na kuongeza kuwa
watakaobainika kutenda kosa hilo la kinyama watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Vitendo vya unyanyasaji na ugomvi baina
ya wafugaji na wakulima vimeendelea kuripotiwa katika maeneo mengi hapa nchini,
hivyo lisipoangaliwa na kuchukuliwa kwa hatua stahiki amani ya Watanzania
itakuwa matatani.
Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment