Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, November 7, 2013

AZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KIFO CHA MWANAE MSHEWE MBEYA VIJIJINI

Hili ndilo kaburi alimozikwa Alson Mwaikasu akiwa hai
Edward Mwaikasu akionyesha kaburi la ndugu yake aliezikwa akiwa hai
Kaburi la Juma Mwaikasu aliefariki kwa ugonjwa wa wa kupooza baada ya kuanguka bafuni
Ndugu wa marehemu wakiwa msibani
Kushoto ni Elisia Kibweja ambae ni mke  wa alison aliyezikwa akiwa hai kulia ni mke wa Juma Mwaikasu Enesia Daliasi 40 ambae mumewe alikufa kwa ugonjwa wa kupooza 
Mtoto wa marehemu aliezikwa akiwa hai Tunosye Mwakabana Mwaikasu

Biashara zikiwa zimefungwa baada ya wenyeji kukumbilia msituni kwa hofu ya kukamatwa  na vyombo vya usalama
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 12  akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mshewe wakituhumiwa kwa kosa la kuua mtu kwa kumzika akiwa hai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa lilitokea juzi majira ya  saa 08:30  mchana  novemba 6 mwaka huu  katika kijiji cha Mshewe, kata   ya  Mshewe , tarafa ya  bonde la Usongwe wilaya ya  Mbeya vijijini Mkoani hapa.

Alimtaja marehemu kuwa ni Alison maarufu kwa jina la  Hanahela Mwakabana(80) kyusa, mkulima, mkazi wa kijiji cha Mshewe ambaye  aliuawa na kundi la wananchi  walioamua kujichukulia sheria mkononi.

Alisema wauaji hao walikuwa  wakiongozwa na   Julius  Katisha Ngole ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Mshewe baada ya  kumfukia ndani ya  kaburi akiwa hai.

Alisema  chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za kishirikina baada ya  marehemu kutuhumiwa kumuua mtoto wake Juma Hanahela(48) kyusa, fundi ushonaji, mkazi wa kijiji cha Mshewe aliyefariki dunia  Novemba 5, mwaka huu kwa maradhi ya  kiharusi ambayo alianza kuugua Oktoba 29, Mwaka huu na kulazwa hospitali teule ya  Ifisi.

Kamanda Diwani alisema mbinu iliyotumika ni  watuhumiwa   baada ya  kumaliza kuchimba  kaburi walimwambia marehemu aingie ndani ya  kaburi ili apime kama linatosha kumzika mtoto wake ndipo walipomfukia, kisha kuchimba kaburi lingine pembeni na kumzika mtoto wake  Juma Hanahela.

Kwa mujibu wa Mjomba wa Marehemu ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo,Edward Mwaikasu aliliambia JamboLeo kuwa wakati taratibu za mazishi ya mtoto wao zinaendelea aliwashauri kumwita mchungaji yeyote wa kanisa lililokaribu jambo ambalo liliafikiwa na Mwenyekiti wa Kitongoji.

Alisema wakati wakisubiri taratibu hizo kufanyika Mwenyekiti alisikika akimtuhumu Marehemu kuwa ndiye aliyemuua mwanae hivyo adhabu inayostahili dhidi yake inaandaliwa na lazima naye ashughulikiwe.

Alisema wakati Mwenyekiti akiongea hivyo waliokuwa wakichimba kaburi kwa ajili ya kumzika Marehemu walimwita wakitaka asaidie kuchimba shimo ambapowalimtaka kuingia ndani ya shimo na kutoa udongo ambapo baada ya kufanya hivyo walianza kumrushia udongo na kumfukia.

Alisema kutokana na tukio hilo Mwenyekiti alishauriwa apige simu polisi akidai kuwa Marehemu alifanya tukio msibani hivyo wananchi wenye hasira kali wamemuua hivyo nay eye kukubaliana na ushauri huo.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia  watuhumiwa kumi na mbili 12 kuhusiana na tukio hili wakiongozwa na Mwenyekiti Julius Katisha Ngole(52) msafwa, wote wakazi wa kijiji cha mshewe.

Kamanda Diwani alisema  taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na pia mwili wa marehemu ufukuliwe na kufanyiwa uchunguzi  wa kitabibu ili uzikwe upya kwa heshima na taratibu zinazopaswa. 

lakini mpaka hivi sasa mwili haujaweza fukuliwa  na pia wananchi wametoweka kijijini hapo hivyo shughuli za kiuchumi kuzorota.


Picha na ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

No comments: