Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 4, 2013

WALIMU WAKOSA CHOO, WAJISAIDIA KWA JIRANI JIJINI MBEYA, MBUNGE DR. MWANJELWA, ACHANGIA UJENZI WA CHOO CHA WANAFUNZI

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,(CCM) Dr. Mary Mwanjelwa, akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Airport, Jijini Mbeya ambako alichangia mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi kama alivyoombwa na uongozi wa shule hiyo.

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa(kushoto), akikabidhi mifuko 20 ya saruji kwa uongozi wa shule ya Msingi Airport, Jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo kama alivyoombwa na uongozi wa shule hiyo.
 Kulia ni diwani wa kata ya Iyela Jijin Mbeya, ndugu Charles(Chadema), akisalimiana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM), Dr. Mary Mwanjelwa alipofika katika shule ya Msingi Airport, shule ambayo ni pacha wa shule ya Msingi Pambogo, ambayo alisoma mwana mziki nguli, Tabia Mwanjelwa, ambaye ni shangazi wa Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa.

 Wanafunzi hoyeeeeeeeeeee.......
 Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Airport, wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya(CCM),Dr. Mary Mwanjelwa, alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambapo alitoa mifuko 20, ya saruji.

Kulia ni Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, baada ya kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi wa shule ya Msingi Airport ya Jijini Mbeya, akisalimiana na Mwalimu''shujaa'',Damari Fidelis Obadia, ambaye ilielezwa kuwa ni Mwalimu pekee ambaye alichangia Tsh.100,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho cha wanafunzi wa shule hiyo.


''Mungu awabariki'' Mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Msingi Airport ya Jijini Mbeya, alipofika kuchangia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambapo alichangia mifuko 20 ya Saruji.


Habari kwa hisani ya Kalulunga Media

No comments: