NA DANNY TWEVE INDABAAFRICA MBOZI
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Mhongo amewataka madiwani nchini kuachana na mitazamo
ya kizamani kuwa kila suala linalohusiana na maendeleo ni lazima lielekezwe
kwenye serikali kuu wakati wao wanakalia rasrimali zinazoweza kutatua kero
hizo.
Akizungumza baada ya
kupokea maswali mbalimbali kutoka kwa madiwani wa wilihohudhulia katika
mapokezi yake wilayani Mbozi, Mhongo amesema ni vyema sasa halmashauri zikaanza
kutenga fedha kwaajili ya kufadhiri miradi ya umeme kama inavyofanyika kwenye
miradi mingine
Alisema hali hiyo
itasaidia kusukuma mbele jitihada za kujiletea maendeleo na hasa kwa kuzingatia
kuwa REA pia imejielekeza katika utekelezaji wa miradi ya umeme wa jua kwaajili
ya maeneo maalum kama shule.
Profesa Mhongo alisema ni
vyema Madiwani kuachana na ziara na safari zisizo na tija kwa halmashauri zao
na kuendelea kutumia vibaya rasrimali za taifa wakati mahitaji ya wananchi ni
makubwa kwenye masuala yanayohusiana na maendeleo hususani Umeme na huduma
zingine
Alitolea mfano miradi ya
umeme wa jua kwenye shule za sekondari zenye madarasa 8 mitambo yake inaghalimu
kiasi cha shilingi millioni nne ambazo halmashauri za wilaya zinaweza kutenga
kwenye mapato yake na kuwaita REA ili wawezeshe ufungaji wa umeme huo.
Aidha akifafanua hali ya
upatikanaji wa umeme nchini Profesa Mhongo amesema kwa sasa hali ya
upatikanaji umeme vijijini ni asilimia 7 na lengo ni kufikia asilimia 20
ifikapo 2015.
Kwa upande wa upatikanaji
wa umeme kwa ujumla nchini alisema asilimia 20 ya watanzania wanapata umeme na
lengo ni kufikia asilimia 30 ifikapo 2015 ingawa msukumo mkubwa unaelekezwa
vijijini
Akitoa takwimu za jumla
Meneja Msaidizi wa ufundi wa REA bwana GISSIMA NYAMBO –HANGA alisema kwa wilaya
ya Mbozi na Momba REA imetenga shilingi Bilion 22 kuwezesha umeme
katika vijiji vya wilaya ya Mbozi
Alitaja baadhi ya maeneo
yaliyopo kwenye mpango huo ni pamoja na Kamsamba, Hasamba, Hatelele, Isansa,
Msanyila, Msia, Nanyala, Senjele, Mbimba, Nkanga, Oldvwawa, Itaka, Itepula,
Ndalambo, Msangano, Hezya na Ivwanga
Alisema wateja wa awali
2700 wataunganishwa na mfumo huo wa umeme na kwamba hatua za kumpata mkandarasi
zipo mbioni na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza November 2013.
Kwa hisani ya DANNY TWEVE INDABAAFRICA MBOZI
|
No comments:
Post a Comment