Mwenge wa Uhuru ukiwasili Jijini Mbeya katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Iwambi ukitokea Wilaya ya Chunya ulikomaliza mbio zake ukiwa umebebwa na wakimbiza mwenge kitaifa. |
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akisoma taarifa ya Mbio za Mwenge ulivyokimbizwa Wilayani kwake kabla ya kumkabidhi mkuu wa Wilaya ya Mbeya. |
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akitamka kiapo cha kumkabidhi Mwenge pamoja na Wakimbiza Mwenge wa Kimkoa na Kitaifa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King. |
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya tayari kwa kuanza kuukimbiza katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iwambi wakisoma Shairi wakati mwenge ukiweka Jiwe la msingi katika jengo la utawala la shule hiyo pamoja na kuona klabu za kupambana na rushwa shuleni hapo. |
Vituko na vichekesho vilikuwa mbele katika kupamba shughuli za Mwenge katika jiji la Mbeya. |
Mradi wa ujenzi wa daraja ulifunguliwa katika kata ya Itende |
Wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na Wanafunzi waliojitokeza kuupokea Mwenge wakiushika kwa karibu kama ishara ya kuutukuza Utanzania |
Nyumba ya Watumishi wa Zahanati ya Mwansekwa iliyopo katika kata ya Mwansekwa ilifunguliwa. |
Mradi wa maji katika kata ya Itagano uliwekewa jiwe la msingi mradi unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Novemba. |
Mwenge wa Uhuru pia ulizindua Ushirika wa wasafirishaji wa Bajaji Jiji la Mbeya katika ofisi zao zilizopo katika kata ya Iganzo. |
Mwenyekiti wa Ushirika wa Wasafirishaji wa Bajaji Mbeya Idd Ramadhani akionesha Hati ya Utendaji bora waliyotunukiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa. |
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Musa Zungiza pamoja na viongozi wengine wakifuatilia kwa makini shughuli zinazoendelea uwanjani hapo. Na Mbeya yetu |
No comments:
Post a Comment