Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 18, 2013

KUMBUKUMBU YA MZEE ASHERI MWASANDUBE‏
MWAKA MMOJA WA MAREHEMU MZEE ASHERI A.M. MWASANDUBE
 
1942 - 2012
 
Siku, miezi na sasa mwaka mmoja umetimiza tangu Mwenyezi Mungu akuite nyumbani.   Alhamisi ya tarehe 11 Oktoba, 2012 ilikuwa ya majonzi makuu katika familia yetu, Bwana alipotazama shambani mwake akaona nafasi, kisha akatazama duniani na kukuona baba yetu mpendwa ukiwa taabani pale Muhimbili Hospitali, ndipo alipokukumbatia na kukuambia ASHERI Mwanangu inatosha njoo nyumbani.
 
Hakika bustani ya Bwana yapendekeza imesheheni watu wake walio bora, wampendezaye.  Nasi tunazidi kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha haya, tangu tulivyokuwa nawe kimwili hadi sasa ambapo unaendelea kudumu nasi kiroho.
 
unakumbukwa sana na familia yako Mama ELESIA KATAPA, Watoto wako Hilda, Sarome, Stephen, Sekela, Abrahamu, wajukuu zako, dada zako, wadogo zako, ndugu, majirani kila mmoja kwa namna ya pekee.
 
Kwetu Baba yetu mpendwa unaendelea kudumu katika kila pumzi ya uhai wetu, tunaendelea kusimama katika misingi uliyoiweka tena bila kutetereka, tukitumaini kuwa siku moja tutaungana nawe katika kiti cha enzi cha Bwana  wetu Yesu Kristo.  "AMEN"
 

2 TIMOTHEO 4:7

No comments: