WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MAGARI MANNE
KUGONGANA NA
KUSABABISHA
VIFO.
|
§
MNAMO TAREHE 26.09.2013
MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA
BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA
KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON MACHA, AKIWA NA TINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA
GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA
YA SCANIA LORI LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL ARON,
MIAKA 30, MBENA, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA
PEMBENI YA BARABARA LIKIWA
LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.
§
AIDHA GARI HILO T.605 AXX /T.480 CAX
LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO
KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ
AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA
LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA
LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O
KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA
MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.
§
KATIKA
AJALI HIYO MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX NA
T.255 AKV/T.272 CDZ YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA
GARI T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA KICHWA UPANDE WA KULIA.
§
CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI
T.605 AXX /T.480 CAX.
§
MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA
ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.
§
MIILI YA MAREHEMU WILSON MACHA NA JUMA SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA KATIKA GARI MWILI WA MAREHEMU SIXTUS
S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA MAGARI ENEO LA TUKIO ZINAENDELEA.
§
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed By:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
PICHA NA MDAU W MBEYA YETU
|
No comments:
Post a Comment