Huyu ndiye Mwenyekti mpya wa Chama cha wasanii mkoa wa Mbeya Samweli Mwamboma
Chama cha wasanii Jiji la Mbeya kimefufua umoja
wao na hatimaye kufanya uchaguzi kupata viongozi watakaowaongoza kwakipindi cha
miaka mitatu katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden Jijini
Mbeya na kusimamiwa na Viongozi wa Jiji la Mbeya akiwemo Afisa kutoka Ofisi ya
Raisi Utumishi, Julius Mwambogela na Afisa Utamaduni wa Jiji Nimwindael
Mjema.
Wasanii wa Chama cha Wasanii Jiji la Mbeya ambao
wamefufua umoja wao baada ya kukaa muda mrefu bila kushikamana licha ya usajili
kufanyika Mwaka 2004 ambapo wametakiwa kufuata malengo yaliyowafanya wajiunge
na umoja huo.
Katika uchaguzi huo jumla ya nafasi Sita
zilichaguliwa zikiwa za Wajumbe Wanne, Mtuza hazina, Katibu Msaidizi, Katibu,
Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti ambao walichaguliwa kutoka kwa wapiga kuru 30
kutoka vikundi 10 vya sanaa ndani ya jiji la Mbeya waliowakilishwa na wajumbe
watatu kila kundi.
Makundi ya sanaa yaliyowakilishwa katika
uchaguzi huo ni pamoja na Tupume, Bantu,Volcano, Kasi Mpya, Sombe, Umbe, UWT
Isanga, Sisi family, Isika, Golden Power na Umoja.
Hata hivyo uchaguzi huo ulifanyika kwa utulivu
mkubwa huku nafasi za wajumbe zikiwa na wagombea wanne ambao wote walipitishwa
kutokana na katiba yao kuruhusu wajumbe wenye idadi hiyo lakini ikihitaji
kupitishwa kwa zaidi ya nusu ya kura.
Akitanaza matokeo ya uchaguzi huo Afisa
Utamaduni wa Jiji, Nimwindael Mjema alisema Wajumbe waliopitishwa ambao kura
zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Chihanga Timotheo (20), Clemence
Dachi(15), Kenny lunguya (25) na rajabu mrisho Rajabu (20).
Alimtangaza aliyeshinda nafasi ya utunza hazina
kuwa ni Peter Mwambala aliyepata kura za ndiyo 21 na kur za hapana 8 baada ya
mgombea pekee wa nafasi hiyohuku nafasi ya Katibu Msaidizi ikinyakuliwa na
Bahati Shulula baada ya kmbwaga mpinzani wake Shabani Lazack kwa kura 27
dhidi ya 2.
Alisema nafasi ya Katibu wa Chama hicho cha
wasanii Jiji la Mbeya imechukuliwa na Ramadhani Shabani baada ya kura 23 dhidi
ya Peter Anton aliyepata kura 5, na nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikiwa na
mgombea mmoja ambaye ni Halima Ntandu aliyepitishwa kwa kura za ndiyo 28 huku
kura mbili zikimkataa.
Nafasi ya Mwenyekiti ilichukuliwa na Samweli
John Mwamboma aliyepita kwa kishindo baada ya kupata kura 29 dhidi ya mpinzani
wake Zwadi Mtavangu aliyejinyakulia kura Moja pekee kutoka kwa wapiga kura
waliojitokeza.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment