Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 7, 2013

Wafanyakazi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (Nssf) Mkoa wa Mbeya wametoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu eneo la Soko matola Jijini Mbeya ili waweze kusherekea sikukuu ya Iddi.


Tunashukuru sana kwa msaada wenu utakaotuwezesha kuwapatia watoto hawa kwenye sherehe ya Idd” alisema Sheickh Abasi Mshauri kwa niaba ya watoto hao wakati akipokea msaada huo

Meneja wa Nssf Mkoa wa Mbeya, Robert Kadege, alisema wafanyakazi wa shirika hilo maeneo mbalimbali wamekuwa na utamaduni wa kujichangia na kuisadia jamii isiyojiweza wakiwemo watoto waishio katika mazingira magumu.




Wafanyakazi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (Nssf) Mkoa wa Mbeya wametoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu eneo la Soko matola Jijini Mbeya ili waweze kusherekea sikukuu ya Iddi.

Msaada huo uliotolewa na wafanyakazi hao wa NSSF ni Mchele kilogramu 160, mafuta ya kupikia plastiki moja, Chumvu katoni moja na Mbuzi wawili.

Watoto hao wapatao 30 wamekusanywa na viongozi wa dini ya kiislamu katika madrasa ya Ittihal iliyopo eneo hilo la  Soko matola.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo wa vyakula vyenye thamani ya shilingi laki sita, Meneja wa Nssf Mkoa wa Mbeya, Robert Kadege, alisema wafanyakazi wa shirika hilo maeneo mbalimbali wamekuwa na utamaduni wa kujichangia na kuisadia jamii isiyojiweza wakiwemo watoto waishio katika mazingira magumu.

Alisema wamekuwa wakiguswa wanaposikia ama kuaona watoto yatima wakiwa wanaranda randa mitaani baada ya kuwakosa wazazi ama walezi.
“Sisi wafanyakazi wa nssf tumekuwa na utamaduni wetu katika kuisadia jamii wakiwemo watoto, hivyo baada ya kupata tarifa kwa kituo hiki kimewakusanya watoto toka maeneo mbalimbali tumeamua kujichanga chochote na kuwaletea ili waweze kupata chakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd” alisema Meneja huyo.

Aidha, Meneja huyo alisema jitihada zinazowafanywa na viongozi wa madrasa hiyo katika kuwapatia watoto hao elimu ni jambo la msingi kwani lengo lake ni kuondakana na taifa lenye watu mbumbuu.

Kwa upande wake heckh wa Madrasa hiyo, Sheickh Abbas Mshauri, alisema kuwa licha ya wao kuwa wanafundisha masuala ya kiislamu lakini pia kimeamua kuwakusanya watoto wote bila kujali itikadi ya kidini lengo ni kuona wanapata msaada wa karibu kutoka kwa wadau.
“Tunashukuru sana kwa msaada wenu utakaotuwezesha kuwapatia watoto hawa kwenye sherehe ya Idd” alisema Sheickh huyo.
    
                                              Na Mbeya yetu

No comments: