Wanafunzi wakivuka katika Nguzo bila kujali hatari ya Mfereji
Wakazi
wa Kijiji cha Kapunga na Wananchi wa Kitongoji cha SiteOne wote wa Kijiji cha
Kapunga Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya, wamejikuta wakigawanyika baada ya
Mwekezaji wa Kapunga Rise Project kujenga Shule ya Msingi kwa ajili ya Matumizi
ya Kijiji hicho lakini kukataliwa na kujenga ya kwao.
Mgawanyiko
huo umetokea baada ya Wananchi wa Kijiji hicho kukataa kuyatumia madarasa
yaliyojengwa na Mwekezaji na baadaye kujenga madarasa mengine ambayo yameanza
kutumika huku baadhi ya Wakazi wa Kitongoji cha SiteOne kugomea madarasa ya
Kijiji na kutaka kutumia Majengo ya Mwekezaji.
Wananchi
wa Kitongoji hicho wamesema hawako tayari kutumia madarasa yaliyojengwa na
Wanakijiji licha ya madarasa yaliyojengwa na Mwekezaji kukosa miundombinu
muhimu kama Madawati na Walimu na kuahidi kuchonga Madawati 75 ndani ya wiki
hili kwa ajili ya Wanafunzi 151.
Hata
hivyo hali bado itabaki katika Sintofahamu juu ya Walimu na Vitendea kazi vya
kufundishia baada ya kumaliza kutengeneza madawati kutokana na Walimu waliokuwa
wakifundisha Shule ya Awali kuhamia katika Shule ya Kijiji.
Wanakijiji
waligomea kutumia Shule ya Mwekezaji ambayo ilikabidhiwa na Meneja wa Shamba
hilo Justine Veemark kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Hussein Kiffu katika
hafla iliyofanyika Julai 5, Mwaka huu na kuhudhuriwa na Afisa Elimu wa Mkoa wa
Mbeya Juma Kaponda, Viongozi wa Elimu ngazi ya Wilaya Mwenyekiti wa Kijiji
pamoja na Wananchi.
Mwenyekiti
wa Kijiji hicho Ramadhani Nyoni amesema wameshindwa kuyatumia majengo hayo
kutokana na kutopata maelekezo yoyote Serikalini kuhusu Wanafunzi wanaostahili
kusoma katika Shule hiyo wakiwemo Walimu hali iliyowalazimu kujenga shule
nyingine kwa manufaa ya watoto wao.
Aidha
Mwenyekiti huyo anakiri kukabidhiwa funguo za shule hiyo lakini haitumiki licha
ya Wanafunzi wanaotoka katika Kitongoji cha Site One kuhudhuria shuleni hapo
kila siku na kuishia kucheza tu kutokana na kutokuwepo kwa madawati na walimu.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa mbali na kugomea kuyatumia majengo hayo pia
hawakushirikishwa kabla ya kuanza kwa ujenzi na kumlaumu Mwekezaji kwa kubadili
matumizi ya Shamba ambalo alipewa kwa ajili ya kilimo lakini yeye kujenga Shule
ndani ya Shamba alilowekeza.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa Juma Kaponda amemshukuru mwekezaji huyo kwa kujenga shule nzuri na kumtaka kuongeza eneo kutoka Ekari 3.8 kufikia 7.5 ambapo mwekezaji amekubali kufanya hivyo.
Hata hivyo Kaponda amemshauli mwekezaji kuhamisha hati miliki ya eneo hilo la shule ili lihamie sasa kweye hati miliki ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Afisa Elimu amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na wazazi wa Site One cha kuwapeleka wanafunzi bila kuwepo kwa walimu shuleni hapo na kwamba wanafunzi watakao soma shule iliyojengwa na mwekezaji ni kuanzia darasa la kwanza hadi la sita kwani wale wa darasa la saba wamesha sajiliwa kwa ajili ya mitihani.
Aliongeza kuwa shule ya wanakijiji itatumia usajili wa zamani na hii mpya itapewa usajili mpya
Picha Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment