Katika
kuonesha Mtandao wa www.mbeyayetu.blogspot.com
unaendelea kutoa habari za kuaminika kote Ulimwengu baadhi ya Wadau wameshauri
kujikita zaidi katika kutangaza vivutio vinavyopatikana ndani ya Mkoa wa Mbeya
ili kuvutia Watalii na wawekezaji kuja Mkoani Mbeya kuwekeza na kuongeza uchumi
na maendeleo ya Mkoa.
Rai
hiyo imetolewa jana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA), Philip Saliboko, alipokuwa akichangia Mada katika Kongamano la
Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya na Wadau lililofanyika katika ukumbi wa Mkapa
Jijini Mbeya.
Saliboko
amesema kutokana na teknolojia kubadilika watu wengi hupendelea kusoma
mitandao ya kijamii ambayo husomwa sehemu kubwa duniani hivyo yanapoandikwa
mambo mazuri ya Mkoa wa Mbeya yatasaidia katika kuinua maendeleo na uwekezaji
wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Ametolea
mfano mtandao wa Mbeya yetu kuwa ukitangaza na kuandika habari za vivutio vya
utalii vinavyopatikana ndani ya Mkoa itasaidia kuwavuta watalii wa kimataifa
kufika na kutembelea vivutio hivyo na hatimaye kyuimarisha utalii wa ndani ya
Mkoa wa Mbeya.
Aidha
kwaupande wake Uongozi wa Mtandao huo katika kujibu changamoto hiyo,
wamekubaliana na ushauri huo na kutoa Wito kwa Wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa
Mbeya kuwasaidia namna ya kuvifikia na kupata historia za Vivutio hivyo ili
viweze kutangazwa.
Hata hivyo wamedai kuwa suala linaloukabili
Mtandao huo ni kutokana na ukosefu wa miundombinu mizuri itakayoweza kuwafikisha
Waandishi wake katika Maeneo mbali mbali ambapo wametoa Wito kwa Halmashauri
zote kusaidia kuwawezesha kuvifikia vivutio vya utalii katika maeneo yao.
|
No comments:
Post a Comment