Mabanda ya wanyama yakiendelea kutengenezwa
**********
Katika kuhakikisha Maonesho ya
Mwaka huu ya siku ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yatakayofanyika Mkoani Mbeya yanafana kuliko
sehemu nyingine wadau mbali mbali wajitokeza kuyapamba.
Hali hiyo inatokana na Maonesho
hayo kupelekwa Mkoani Dodoma kitaifa kwa Mwaka wa Sita mfululizo hivyo
kuwafanya wakazi wa Nyanda zsa Juu kusini kuonekana kama wamesusiwa hivyo
juhudi za maksudi zinafanyika ili kuyanogesha kuzidi ya kitaifa.
Baadhi ya Makampuni
yaliyojitokeza na kujidhatiti kuyapamba maonesho hayo ni pamoja na Kampuni ya
Vinywaji baridi ya SBC (T) LTD kupitia
vinywaji vyao vya Pepsi na Mountain Dew ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Maonesho hayo kwa mwaka huu.
Kampuni nyingine iliyojitokeza
ni MLM International Vision (T) LTD ya jijini Mbeya ambayo Mwaka huu
imedhamiria kuleta wanyama hai kwa lengo la kukuza utalii wa Ndani ya nchi na
kuwasaidia Wananchi ambao hawana fursa za kutembelea mbuga za Wanyama na
Vivutio vya Nchini Tanzania.
Akizungumzia mikakati ya
Kampuni hiyo, Afisa Uhusiano wa MLM, Venance Matinya, amesema Wanyama
watakaoletwa ni pamoja na Simba Jike, Simba Dume, Mbega, Chui na Chatu ambao
watu mbali mbali watapata fursa za kujua historia zao pamoja na mafunzo mbali mbali kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii.
Matinya ameongeza kuwa Wanyama
hao watatumika kama mabalozi wa kutangaza utalii wa ndani na Mijini, ambapo pia
ndani ya mabanda ya Wanyama kutakuwa na shughuli mbali mbali hivyo
wajasiliamali wanakaribishwa kuuza bidhaa ndogo ndogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Kampuni hiyo, William Mkandawile, amesema wahusika wa Wizara ya Maliasili na
Utalii pamoja na makampuni yanayojihusisha na utalii kuzisaidia sehemu husika
kutangaza ili wananchi wapende kutembelea vivutio vilivyokaribu nao.
No comments:
Post a Comment