Wakazi wa Wilaya ya
Ileje wanaoishi mikoa ya Iringa,Njombe,Rukwa na Mbeya Mjini,kwa pamoja
wamemuomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuona umuhimu wa
kubadilisha mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya iliyopendekeza
makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe yawe eneo la Mkwajuni wilayani Chunya,kwa
madai kuwa ni mbali ukilinganisha na Jiografia ya wilaya ya ileje.
Wananchi wa wilaya
ya Ileje wametoa maombi yao wakati wa Kongamano lililoshirikisha wakazi wa
ileje wanaoishi Nje ya wilaya hiyo,lililofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel
Jijini Mbeya,wakijadiliana maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na mgawanyo wa
mkoa wa Mbeya na kupata mkoa mwingine mpya,ambao wameomba mapendekezo ya makao
makuu ya mkoa huo yasogezwe.
Wakizungumza katika
Mkutano huo Wananchi hao wamedai kuwa umbali kutoka Wilayani Ileje kwenda Mbeya
Mjini ni mbali sana hivyo kuwapeleka Mkwajuni ni kuzidi kuwaongezea safari
zaidi.
Yohana Seme
Mkazi wa Ileje amesema lengo la kugawanya Mkoa ni kusogeza huduma kwa
Wananchi lakini Mapendekezo ya Kupeleka Makao makuu ya Mkoa Wilayani Chunya ni
kupokonya huduma kwa Wakazi wa Ileje ambao huduma nyingi hutegemea Nchi jirani
ya Malawi.
Mjadala wao
wanaileje ukaenda mbali zaidi,baada ya mapendekezo ya awali ya wajumbe wa
kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya,kupendekeza makao makuu ya mkoa wa Songwe
yawe ni Mkwajuni Kilometa 321 kutoka kusini mwa wilaya ya Ileje.
Kutokana na umuhimu
wa Kongamano hili,Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona ambaye pia
alikuwepo katika Mkutano huo alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko
tayari kukubaliana na maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya.
Kibona amesema mapendekezo
ya Wanaileje ni kwamba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe yasogezwe na kuwekwa
katika kijiji cha Henje wilayani Mbozi, mapendekezo ambayo yameungwa Mkono na
Wakazi wa Momba, Mbozi na Ileje yenyewe.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
KUNA HAJA YA KUANGALIA VIZURI WALIOSHIRIKI KUTOA MAAMUZI HAYO KWA KUJILIZA YAFATAYO;
(i) NI KWELI WASHAURI WALIANGALIA SUALA LA UMBALI KATI YA MAKAO MAKUU YA MKOA NA MAENEO TAWALIWA?
(ii) uzalendo ulikuwepo wakati wa kufanya maamuzi haya? kwani hili limeisogeza Ileje Malawi zaidi ya ilivyokuwa mwanzo....
(iii)kwanini Mkuu wa Mkoa amekuwa mzito kufikiria upya maoni ya wanaohusika na mkoa wenyewe kwa kuangalia matakwa ya wengi kuliko afanyavyo sasa ambapo inaonesha mbali tu na kuwepo dalili za RUSHWA pia kuna kila dalili ya kutumiwa na watu fulani, binafsi sina imani na Mkuu wa Mkoa....
(iv) hili halihitaji Elimu kubwa kulifahamu, Wapi kuna idadi kubwa ya watu, wapi kijiografia ni katikati ya mkoa? wapi kutakuwa ni rahisi kuhudumia maeneo yote kwa urahisi?
acha niishie hapo, MKUU WA MKOA NA KAMATI YA USHAURI MJIPANGE
Ileje itakuwa mbali zaidi na makao makuu ya mkoa wake mpya kuliko mwanzao. Nadhani kuna walakini katika uelewa wa kijiografia kwa waliofanya maamuzi. Pia sioni sababu kwa nini makao makuu yawe Mkwajuni ambako ni vigumu kufika na ni mji mdogo ambao utahitaji fedha nyingi kuuweka katika hali ya makao makuu, wakati vwawa, ambao kijiografia umekaa katikati, ya Mkwajuni na Ileje, tayari una miundombinu inayouweka katika hali ya kufaa kuwa makao makuu. Kuna nini hapa kinachopelekea Mkwajuni kuwa makao makuu? Ni kitu kinachoshangaza wengi, na si watu wa ileje tu. Fikirini vizuri mnaohusika, isije kuwa ufisadi unasababisha haya.
Post a Comment