Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 16, 2013

MAANDALIZI YA SIKUKUU YA MAONESHO YA WAKULIMA (NANENANE) KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YAKAMILIKA.

 Meneja wa uwanja wa John Mwakangale wa maonesho ya Nanenane Kasilati Mwakibete akiwa katika ziara ya kuangalia maandalizi ya Nanenane



 Waandishi wakiwa kwenye Ziara



 Shughuli Mbalimbali zikiendelea
 Mkaguzi msaidizi wa Magereza Daniel Wabare ambaye pia ni  msimamizi wa  Banda la Magereza Nane nane   akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.


Hatimaye maandalizi ya maonesho ya sikukuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yatakayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Uyole Mkoani Mbeya yamekamilika kwa asilimia Miamoja.

Akizungumzia hali ya maandalizi ya maonesho hayo kwa Mwaka 2013, Meneja wa Uwanja huo Mwakibete Kasilati amesema hadi sasa baadhi ya Washiriki wameshaanza kufanya shughuli zao kama kawaida.

Amesema Mwaka huu  kunahamasa kubwa sana tofauti na miaka ya nyuma ambapo Wafanyabiashara wengi wamejitokeza hivyo kuenea uwanja mzima mapema.

Amesema kuna maeneo ambayo hayakuwahi kutumika kutokana na baadhi ya washiriki kujikusanya sehemu moja ambapo ameongeza kuwa safari hii hali hiyo haitakuwepo baada ya kutawanyika kila upande.

Aidha baadhi ya mabanda yaliyotembelewa yalionekana kuendelea na shughuli zao ikiwa ni pamoja na kufanya usafi, kuboresha bustani na ukarabati mdogodogo.

 BOFYA HAPA READ MORE KUSOMA ZAIDI
 
Mabanda yaliyotembelewa na kutia hamasa kwa washiriki wa Mwaka huu ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya kuoneshea Wanyama hai ambao ni Simba, Chui, Mbega, Kobe na wengine kibao.

Mabanda mengine yanayoendelea na kazi ni pamoja na banda la Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) huku baadhi ya vibanda vya Chakula (mama ntilie) na grosari zikiendelea na shughuli zao.
















 Maeneo Mbalimbali
 Mmoja wa waandishi akiwa anapiga picha mambo mbalimbali





Picha zote na Mbeya yetu 


**************************



No comments: