Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 29, 2013

JIJI LA MBEYA LAWAMANI KWA KUSHINDWA KUSAWAZISHA VIFUSI KWA WAKATI, KUKWEPA KUBOMOA MAJENGO YALIYO BARABARANI.

Vifusi vikiwa katikati ya barabara ya Mwaji na Stendi ya Tazara Uyole Jijini Mbeya vinavyodaiwa kutelekezwa kwa zaidi ya wiki mbili. 
Banda la Makuti ambalo lipo nje ya uwanja wa nane likiwa katikati ya Hifadhi ya Barabara ya TanZam na barabara inayojengwa na Wachina na kusababisha kuikwepa kutokana na kushindwa kuibomoa.
Barabara ikionekana kukunja kona kukwepa jengo hili linalodaiwa kumilikiwa na kiongozi mkubwa Mkoani Mbeya.
Jengo linalodaiwa kujengwa kinyemela likiwa ndani ya hifadhi ya barabara na kutoa shoo mbaya kwa uwanja wa nanenane.
Huu ndiyo muonekano wa Jengo hili ambalo licha ya kuwa Barabarani pia ni Uchafu wa Mandhari ya Uwanja wa Nane unaotarajiwa kutumika katika maonesho ya Sadc mwaka 2016.
Barabara ikiwa imepita karibu kabisa na ukuta wa nyumba hii lakini wataalamu wanaiangalia kama hawapo vile.
Mitambo ya wachina ikishindwa kuendelea na kazi kutokana na majengo kuachwa kwenye hifadhi ya barabara wanayoijenga.


Wakazi wa kata ya Itezi Jijini Mbeya wameilalamikia Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kitendo cha kufunga Barabara kuu itokayo Mwaji kuelekea Stendi ya Tazara Uyole.

Barabara hiyo imefungwa kutokana na Halmashauri hiyo kumwaga vifusi katikati ya barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa wenye magari ambao kutokana na hali hiyo wamelazimika kuyaacha magari yao na kutembea kwa miguu.

Kwa mujibu wa taarifa za wananchi wa kata hiyo wamesema hali imedumu kwa zaidi ya Wiki mbili na kusababisha kukata mawasiliano jambo ambalo ni hatari kama kutahitajika huduma ya dharula ya kuhitaji gari kama zimamoto, Tanesco na Ambulance kwa wagonjwa.

Aidha wamehoji kuwa kuna ulazima gani wa kumwaga vifusi kama hawako tayari kuanza kusambaza hali inayosababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo na bila kutoa njia mbadala ya kutumia kabla ya kusawazisha.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwepo kwa mapungufu mengi katika kitengo cha Makandarasi wanaohusika na barabara katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kuwepo kwa maeneo mengi ambayo vifusi huachwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kuonekana kufeli kwa Kitengo hicho pia kunadhihirishwa na ujenzi wa Barabara ndogo ya Lami inayopita pembezoni mwa Uwanja wa Nane nane ambapo Mkandarasi ameanza vizuri kuichonga lakini baadaye akalazimika kupunguza vipimo ili kuyakwepa baadhi ya majengo yanayodaiwa ya Vigogo ndani ya Mkoa wa Mbeya.

Pia kinachoonekana ni kama mchezo wa Panya wa “ nani amfunge paka kengere” kutokana na baadhi ya taasisi zinazohusika kushindwa kutoa amri ya kuvunja majengo hayo licha ya kupita kwenye hifadhi ya barabara pia yanatoa picha mbaya ya Uwanja wa Nane nane.

Baadhi ya watu waliohojiwa wamedai kuwa labda Waziri Magufuli akiingilia kati ndipo majengo hayo yatakapobomolewa na kudai kuwa huko ni kumsumbua Waziri kutokana na majengo hayo kuweza kudhibitiwa na Halmashauri husika.

Picha na Mbeya yetu

No comments: