Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 11, 2013

ALIYE TUMBUKIZA KICHANGA CHOONI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA. (TUNAOMBA RADHI KWA BAADHI YA PICHA ZITAKAZO ONEKANA)

 Rukia Haruna (31) pichani aliye kutwa na hatia ya kutupa mtoto chooni.
 Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela


****************************
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA JUNI 14 .2013 ENEO LA MANGA A JIJINI MBEYA





*********************
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
 
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
 
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
 
Na  Mbeya yetu

6 comments:

YA-TOIVO JAK said...

Sasa tofauti yake huyu dada na muuaji iko wapi...miaka mitano?...kwani kuua kuna excuse yoyote kweli? yaani wtu wanatafuta watoto wengine wanawatupa kweli jamani....Mungu ana macho na hutoa kwa awapendao, lakini ndio maana bibilia inasema "ole wake amtegemeae mwanadamu kwani hataona mema yajapo" huyu dada atakuwa aliweka mategeeo yote kwa aliempa mimba...mema ya Bwana yalipokuja yaani baraka ya kupata mtoto yeye hakuiona kuwa ni baaka badala yake akaona ni takataka...Mungu amsamehe...natamani huyo mtoto angekuwa hai jamani....!!!!!1

Unknown said...

NIKWELI KABISA ANGEPIGWA MIAKA 6

Unknown said...

NIKWELI KABISA ANGEPIGWA MIAKA 6

Anonymous said...

Haijalishi alimtegemea mme wake au la! Yeye ndo aliingia leba na yeye ndo anajua uchungu wa mtoto si huyo mwanaume! Kama aliona hawez kumlea alishindwa nini kumpeleka hata kanisan masister wakamlea! Hapo angeonekana anania njema kuliko kumtupa chooni! Kuna watu hawana akili timamu na hawajielewi! Kweli mwanamke ulielea mimba miez 9 ukazaa kwa uchungu leo unatupa mtoto?? Pumbav sana

Anonymous said...

mm nimeishia kulia tu,roho inauma sana mm huu mwaka wa saba sasa natafuta mtoto bila mafanikio tena leo hii nimetoka hospital kwenye vipimo, leo mwanamke mwenzangu anatupa mtoto tena bila huruma wala aibu? Natamani huyo mtoto ningepewa mm. Mungu atusamehe kwa kweli

Anonymous said...

Mungu atakujalia utapata wako hata Uzeeni! Mkumbuke sara na abraham walipata mtoto lini?? Mungu anatoa kwa wakati na Muda wako utafika mpz utabeba mwanao, walaaniwe watupao watoto jaman