Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 2, 2013

AFUNGWA MIAKA 20 JELA KWA KOSA LA KUGHUSHI NA KUIIBIA BENKI



 Mtuhumiwa wa Kuiba na kugushi Deogratius Mpembe akiwa anatoka mahakamani baada ya kufungwa kifungo cha Miaka 20

 Mtuhumiwa  wa Kesi ya Kuiba na Kughushi  Benki akiondoka Mahakamani
**********************
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mpembe amehukumiwa kutumikia kifungo cha Miaka 20 Jela kwa kosa la kughushi nyaraka za kutolea fedha katika Benki ya CRDB Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, baada ya kumtia hatiani Mshtakiwa kwa makosa 14 ambayo  Mtuhumiwa alikubali kutenda baadhi ya makosa na mengine kuyakanusha.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Lugano Mwakilasa aliiambia mahakama hiyo kuwa Mshtakiwa alitenda makosa hayo katika vipindi tofauti kati ya Mwezi Juni, 2011 kinyume cha kifungu cha 235 Sura ya 20 ya Mwaka 2002 ya kanuni ya adhabu.
Mwakilasa alisema Mtuhumiwa alipatikana na Kosa la kughushi nyaraka za kutolea fedha katika Benki ya CRDB katika akaunti mbili za mteja wa benki hiyo ambaye ni marehemu Clemence Kihanga ambaye imedaiwa mahakamani hapo kuwa na uhusiano na Mshtakiwa.
Mbali na kosa hilo Mtuhumiwa huyo pia  anadaiwa kuiibia Benki hiyo fedha za kigeni Dolla za Marekani 118,137.4 pamoja na fedha za kitanzania Shilingi Milion 2,468,181.24  ambapo Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo akiwa ni karani wa Benki hiyo akiwa na kitambulisho  cha kazi chenye namba CK 4M.
Upande wa Mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambao ni Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanjelwa Ephraim Luwila, Mtaalamu wa maandishi kutoka Jeshi la Polisi namba E2912 Johanes, Mke wa Marehemu Niku Kihanga na Kaimu Meneja wa Benki hiyo Alfred Basajile.
Katika maelezo yao Mashahidi hao walitoa Vielelezo mbali mbali mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi ikiwemo Kitambulisho cha kazi cha Mtuhumiwa, Hati ya Kifo cha marehemu aliyefariki Novemba 2010 na Nyaraka za maandishi ambazo zote zilikuwa na miandiko inayofanana na Mtuhumiwa kama vile Mkato na Sahihi zake.
Awali ilielezwa kuwa kugundulika kwa wizi wa fedha hizo ni baada ya Mke wa Marehemu Niku Kihanga kufuatilia masalio ya akiba ya Mume wake baada ya kuidhinishwa kuwa msimamizi wa mirathi na kuomba kupewa masalio ya akiba zote na kukuta kuna upungufu wa Dola 5000 kwa akaunti ya fedha za nje na akaunti ya ndani ikikutwa na Shilingi 36,000/= badala ya Shilingi 2,400,000/=.
Mke wa marehemu alisema kufuatia kuwepo kwa upungufu mkubwa wa fedha hizo aliamua kupeleka malalamiko kwa Meneja wa benki hiyo ambaye alianza kulifanyia kazi kwa kupeleka malalamiko Polisi.
Kutokana na Ushahidi huo pamoja na maelezo  ya kukiri Polisi,  Hakimu Gilbert Ndeuruo alimtia hatiani Mtuhumiwa kwa makosa yote 14 na kumhukumu kila kosa kwa miaka Mitano ambapo alisema Mtuhumiwa atatumikia makosa yote kwa pamoja kwa kwenda Jela Miaka 20.
Aidha kabla ya kutoa hukumu hiyo Mwendesha mashtaka Lugano Mwakilasa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wasiokuwa waaminifu.
Hata hivyo Hakimu huyo kabla ya kutoa hukumu alimtaka Mtuhumiwa huyo kujitetea ili apunguziwe adhabu ya kifungo cha maisha kutokana na makosa aliyokutwa nayo, ambapo Mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kile alichodai anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa, Mtoto mmoja, Mkewe na Mdogo wake ambaye anamsomesha kuwa wanategemea msaada wake.
Pamoja na utetezi huo ambao Hakimu aliridhika nao na kumpunguzia adhabu kutoka Kifungo cha Maisha hadi kumfunga kutumikia Jela kwa Miaka 20 na kuongeza kuwa anaruhusiwa kukata rufaa endapo hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa ndani ya Siku 30.
PICHA , HABARI NA MBEYA YETU BLOG

2 comments:

Anonymous said...

So sad huyu bwana tumesoma naye chuoni TIA Dar, akafanikiwa kupata kazi ndo akafanya haya yaliyomharibia maisha yake moja kwa moja. inasikitisha sana

Anonymous said...

aah Deo, myroommate!! chozi limenitoka kwa hii habari!! Jamani just easy like that kuona degree yako inaenda kutumikia jela 20 yrs!!!. Jamani Tulioko nje na tunayaona haya, Tukumbuke ni kazi rahisi sana kubomoa Maisha uloyajenga kwa taabu ya miaka mingi. Tukumbuke nyumba imara haijengwi siku moja, inajengwa kwa hatua na kwa uangalifu. Rushwa, wizi, na mafanikio yoyote yasiyohalali ni hatari kwa maisha yetu.

GUYS I MEAN IT FROM MY HEART.