WATUMISHI wa Shirika la Umeme Nchini( Tanesco)
wameaswa kufanya kazi zinazohusu Shirika hilo pekee na siyo kujihusisha na kazi
za Ukandarasi, hali inayosababisha mgongano wa Maslahi kato yao na Wakandarasi.
Aidha imeelezwa kuwa Mtumishi atakayebainika
kujishughulisha na kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na Mkandarasi ajitoe kabisa
katika Shirila ka Tanesco ili aendelee na kazi hiyo ambapo pia Wakandarasi
wanajiingiza katika Shughuli za Tanesco pia wameatakiwa kuacha.
Agizo hilo lilitolewa na Meneja wa Tanesco
Mkoa wa Mbeya Injinia Amos Maganga katika Mkutano wa Uongozi wa Tanesco Mkoa wa
Mbeya na Wamiliki wa Makampuni ya Ukandarasi wa Umeme na wanachama wa Chama cha
Wakandarasi wazawa Tanzania wa Mkoa wa Mbeya (TLCO) uliofanyika katika ukumbi
wa Mkapa Jijini Mbeya.
Aidha katika Mkutano huo ambao awali Raisi wa
Chama cha Wakandarasi Wazawa Tanzania (TLCO) Kura Mayuma, alisema Tanesco na
Wakandarasi ni wadau muhimu wa kumsaidia Mwananchi lakini wanashindwa kufikia
mwafaka kutokana na kuwepo kwa Changamoto.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na
kutokuwa na Mahusiano mazuri kati ya Wakandarasi na Watumishi wa Tanesco,
Watumishi wa Tanesco kufanya kazi za Umeme sambamba na wakandarasi ambapo
alisema Chama kimepata malalamiko kuwepo kwa watumishi ambao huchukua na
kufanya kazi za kikandarasi.
Alisema kutokana na kuingiliana huko kunawafanya
Wakandarasi kuishi maisha ya kuviziana kwa kuwa wateja wengi hasa vijijini
humwamini zaidi Mtumishi wa Shirika kuliko Mkandarasi ambaye ndiye mwenye
jukumu la kutengeneza umeme.
Changamoto zingine ni Vifaa vya kufanyia kazi
kutotosheleza, Mamlaka zingine za Kiserikali kama Tamesa, Nhc, Wakala wa
majengo, Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji kufanya kazi za Wakandarasi,
upimaji wa Service line kuwa na kasoro, Vishoka, kutotambuliwa kwa Wakandarasi
na ofisi ya Tanesco.
Zingine kutokupewa kazi za kusambaza umeme
(kujenga service line), upendeleo wa ajira, kitengo cha umeme wa dharula
kuchelewa kufika eneo la tukio na Malalamiko ya wateja kuwa Shirika
haliwamilikishi moja kwa moja wateja mali wanazolipia.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya
Injinia Amos Maganga, alikijibu baadhi ya Changamoto hizo alisema Tanesco na
Wakandarasi wote kwa pamoja wanadhana moja ya kuhakikisha mteja wanatendewa
haki.
Alisema ili kurudisha mahusiano mazuri kati ya
Watumishi wa Tanesco na Wakandarasi ni pamoja na kukutana mara kwa mara
kwa kufanya mikutano ambapo katika Mkutano huo iliadhimiwa kukutana kila baada
ya miezi 6.
Maganga aliongeza kuwa Mahusiano pia yatakuwepo
endapo Mkandarasi atafanya kazi yake bila kuingilia majukumu ya Tanesco kama
vile Watumishi wa Tanesco kutengeneza umeme hadi kwenye mita na siyo kuingia
ndani ya nyumba ya mteja.
Pia alisema Wakandarasi hawaruhusiwi kupanda
kwenye nguzo na kugusa mita kwa kuwa jukumu hilo ni la wataalamu wa Tanesco na
kuongeza kuwa iwapo Mkandarasi atakutwa kwenye nguzo atachukuliwa hatua kama
kishoka wa umeme.
Alisema baadhi ya Wakandarasi kuhusishwa na wizi
wa Umeme ambapo baada ya kukamatwa kwa wezi huwataja wao, pia kupitisha kazi
zisizokuwa na sifa, Mihuri yao kutumika vibaya na kujengwa laini zisizohalali
na kupitishwa na Mkandarasi bila kupitia taarifa Vizuri.
Aliongeza kuwa Changamoto nyingine inayofanywa na
Makandarasi ni ulanguzi wa Fomu ya Maombi ya mteja ambazo huziuza kati ya
Shilingi 50,000/= na 80,000/= ili hali bei hali ni Shilingi ni kati ya 6000/=
na 10,000/=.
Hata hivyo kutokana na kukithiri kwa hali hiyo
Meneja huyo alisema baadhi ya Wakandarasi wameacha kazi zao na kujishughulisha
na ulanguzi wa Fomu hivyo kuagiza kuwa Mkandarasi hata husika na kumchukulia
fomu mteja.
“ Kuanzia leo nasema Mteja akiwa na picha yake
atanunua fomu ndipo atakapomtafuta Mkandarasi kwa ajili ya taratibu zingine
maana hii tabia imesababisha hata fomu kuisha mapema kutokana na baadhi yao
kuhodhi fomu nyingi na kuzunguka kwenye makorido ya Ofisi za Tanesco ili
kuvizia wateja” alisema Meneja huyo.
Aidha aliwahimiza Wakandarasi kuheshimu ofisi zao
kwa kutulia na kusubiri wateja na siyo kuwavizia wateja kwa kuwalangua bei ya
Fomu na kumlazimisha kumfanyia kazi.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment