Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 13, 2013

REDD'S MISS MBEYA APATIKANA
















HATIMAYE  Mkoa wa Mbeya umepata mwakilishi wa kushiriki kinyang’anyiro cha  Mrimbwende wa Redds Miss Tanzania baada ya shindano la kumpata  Miss Mbeya kukamilika.

Mratibu na Mwandaaji Miss Redds Mkoa wa Mbeya Gabriel Mbwile amesem jumla ya warembo 12 wameshiriki kinynganyiro hicho tangia wawekewe kambi hadi  siku ya shindano.

Ameongea kuwa mshindi wa kwanza amezawadiwa kitita cha fedha taslimu Milioni moja, mshindi  wa pili 750,000/=, mshindi wa tatu 500,000/= na wengine wote wamepewa  kifuta jasho cha  shilingi 100,000/=.

Amewataja washindi hao kuwa ni Jackline Luvanda mshindi wa kwanza, Aneth Brayton mshindi wa pili na Daina  Athlimani aliyeibuka msindi wa tatu.

Amewatja washiriki wengine kuwa ni Naba Magambo, Zainabu Matabi, Salma Abdalah, Flaviana Sixbert, Sarah Samwel, Aisha Beneka, Darlin Athani, Mwajabu Ngobai na Neema Raymond.

Aidha Mgeni rasmi katika kinyang’anyiro hicho  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Diwani Athumani, amezidi kusisitiza suala la amani kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba inapaswa kushughulikiwa ni kila mtu.

PICHA NA MBEYA YETU 


No comments: