Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakifuatilia kwa umakini kikao hicho wakati kikiendelea
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.
Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro unao endelea Chuoni hapo
***************
HALI si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
(TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na
wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula,
Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai
Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa
Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Block T
kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo
mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo
inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani
inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji
wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na madai ya
Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula
inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye barua hapo chini lakini habari kamili
itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.
PICHA , HABARI NA MBEYA YETU
3 comments:
Mhhhh. Hali ni tete. Ila hii lugha iliyotumika sio ya ki-academician kabisa
jamani haya mambo yanayoelezwa kwenyeblog hii nikweli na si kwa walimu tu mambo haya ya ukandamizaji yanafanyika hata kwa wanafunzi wanakandamizwa sana tena sana yani mwanafunzi adai haki yake pale ambapo hajatedewa haki yake mwanafunzi huyo hana chuo. kwa taarifa fupi mwaka 2010 kunawanafunzi walifukuzwa kwa kusingiziwa kwa kile kinachodaiwa eti wamekutwa na madaftari kwaente chumba cha mtihani wasiopungua 25. mwaka uliofuata wanafunzi wasiopungua idadi hiyo nao tena walifukuzwa chuo kwa kuwa tu ni WASABATO NA HAWAKO KUHUDHURIA MIHADHARA NA HATA MITIHANI SIKU ZA JUMAMOSI wakati prospectus ya TEKU inaonesha makundi ya aina hiyo yatakua fevad we mwanateku anagalia ukurasa wa pili utayaona haya. mwaka huu 2013 wamekuzwa WASABATO Wengine wanaozid idadi tajwa apo juu lakin yote haya yafanyika huwa hawatangazi kwamba tumewafukuza kwa kosa gani isipokua kwa wale wa mwaka 2010. mwaka wa tatu di leo hawajpewa fedha zao za utafiti ukiwauliza chenga tupu. njo kwaenye matokeo sasa mama yangu utasema wanaosimamia idara ile nipofu kozi usiyisoma ndo wapewa. mwaka huu kwa mujibu wa TCU pass mark zinatakiwa zianzie 40 wakati nyuma tulikuwa tunafaulu kwa 50, sasa kkasheshe inakuja kwenye cheeti wanachosema watatoa eti kitakua na matokeo ya aina mbili hapa iko ivi! cheti kitaonesha ufaulu wa 50 na pia ufaulu wa 40 sijajua cheti hiki kimataifa kama kipo mtaniasaidia wazangu. tumeoooomba ilo hajakubali kubadilisha ok fine tumekubali cha kushanga na kuchekesha wanafunzi wameoma provision eti zinaoneshatena ufaulu wao ni 40 kuanzia semista 1-5, kuuliza vipi mzee aaah! TUMEKOSEA tunaomba wale walochukua warudishe, wameenda chukua tena mambo ni yale yale basi wao ni KUKOSEA TUUUUUUUUUUU!. HII NDO TEKU
AAAH! HAO TEKU WAMEZOEA TUNAPEWA TARIFA NA NDUGU ZETU WANAOSOMA APO MBEYA HATA UONGOZI WA SEREKALI YA WANAFUNZI ULIOPO NI KWA MASLAHI YA UTAWALA SI KWA MASLAHI YA WANAFUNZI WENYEWE. MFANO MZURI NI MWAKA JANA YAANI 12-13 ALICHAGULIWA RAIS WA CHUO AMBAYE WANAFUNZI WAOTE WAMEMKUBALI HUYU ATATUSAIDIA MATATIZO YETU KWA KIASI FULANI UONGOZI ULIBATILISHA UCHAGUZI ULE KWA KILE KINACHODAIWA KUA ETI MGOMBEA NI CHADEMA MARA OOH ALIFUMANIWA NA MKE WA MTU ILIMRADI TU BADAE TUKAAMBIWA WAMERUDIA UCHAGUZI AMESHINDA MTU AMBAE KWENYE USAHILI TUME ILIMUONDO KWAMBA HAKUWEZA KUFAULU USAILI NA NDIE ALIE SHINDA URAIS, HAKUTOSHA HIYO HAT MWAKA HUU NA HILO LIMEJIRUDIA TENA UCHAGUZI UMEFANYIKA KWA KIJANA AKASHINDA KWA KURA ZAIDI YA 800 BAADAE TUME IKABATILISHA UCHAGUZI KWA KAWAIDA AMRI TOKA UONGOZI NA BAADAE WANAFUNZI WAKATANGAZIWA UCHAGUZI UPA KWAKWELI WLIGOMA KUPIGA KURA CHA KUSHANGAZA TUNA ULIZA NANI AMESHINDA TENA WANATUAMBIA WANAOMTAKA WAO NA ALISHINDA KWA KURA 999 ZAIDI YA WAKWANZA NA HALI WANAFUNZI UCHAGUZI WAPILI WALIGOMA. KWA HIYO JAMANI HEBU KIFATILIENI CHUO HICHO KUNA JAMBO BAYA LINAFANYIKA HAPO MANA KIMSINGI VIONGOZI WA NCHI WANAZALIZALISHWA MAVYUONI SASA KWA HALI HII TUNAMASHAKA NA UONGOZI HUO JAMA TUSAIDIENI VIJANA WAPATE HAKI ZAO KAMA KWELI TUNAHITAJI WASOMI NCHI HII.
Post a Comment