Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, May 17, 2013

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.

Mwenyekiti wa Uwt  Mkoa wa Mbeya Prisila Mbwaga alisema kama Wanawake wa Chama cha Mapinduzi hawako tayari kuona matusi yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete kwamba anachangia kuibomoa Nchi.
 Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete  na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani.
 
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.


Matamko hayo yalitolewa  na Wenyeviti hao katika Mkutano na Vyombo vya habari uliofanyika katika Ofisi za UVCCM Mkoa wa Mbeya, ambapo walisema kamwe hawawezi kufumbia macho maneno ya uzushi na uchonganishi kati ya Serikali na wananchi.
  
Akisoma tamko Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete  na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani.

Alisema katika Mkutano alioufanya Mei 12, Mwaka huu Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya Dk. Slaa akihutubia wananchi kuwa Raisi Kikwete ni Freemason,  Mdini, Mawaziri hawamsaidii pia ni Mafisadi na kuongeza kuwa ana ushahidi wa  Cd ambazo Raisi Kikwete akihamasisha udini na kuhusu uchinjaji.

Alisema maneno ya Dk. Slaa ni uzushi ambao unalengo la kufitinisha Watanzania na Serikali ya Chama cha Mapinduzi hususani anapofanya mikutano ya Hadhara katika Mkoa wa Mbeya ambapo aliongeza kuwa Ufisadi anaousema yeye kwa Mawaziri wa Ccm ili hali yeye mwenyewe anaongoza kwa ubadhilifu wa fedha za Wananchi.

Alitolea mfano wa ubadhilifu uliofanywa na Chadema mkoani Mbeya kuwa ni pamoja na Kitendo chaMwenyekiti wao Freemani Mbowe kuchangisha fedha Milioni Tatu kwa wananchi kwa kile alichodai zingetumika kununulia maji na matibabu wakati wa maandamano lakini hazikufanya kazi hiyo na hazijulikani zilipo.


Kajuna alisema mbali na fedha hizo kutokujulikana matumizi yake  pia Dk. Slaa alichangisha fedha zingine Shilingi Laki saba kwa ajili ya posho ya Wabunge waliofukuzwa bungeni jambo ambalo lilileta sintofahamu kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.


Alisema ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Chadema ambao kila Mwezi wanapata ruzuku ya takribani Milion mia Tatu lakini hawajawahi kujenga hata chumba kimoja cha Zahanati wala kutoa msaada kwa wananchi wasiojiweza lakini wao wanazidi kuwachangisha wananchi.


“ Jamani watanzania fungukeni muone huyu kiongozi wa namna gani Mlafi, Mchoyo na mchochezi  asiyependa kuona amani ya Nchi ikistawi” alisema Kajuna.


Aliongeza kuwa pamoja na Chadema kupata fedha zote hizo bado zinaishia mikononi mwa watu wachache hususani Dar Es Salaam ambapo Mikoani hawazipati na ndiyo sababu Ofisi za Chadema Mkoa wa Mbeya zilifungwa kutokana na kutolipia pango la Nyumba deni la Shilingi Laki tatu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uwt Prisila Mbwaga alisema kama Wanawake wa Chama cha Mapinduzi hawako tayari kuona matusi yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete kwamba anachangia kuibomoa Nchi.


Alisema Shumbusho alinukuliwa akitoa matusi makubwa dhidi ya Mama Salma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Mbozi akisema ameshindwa kumshauri raisi kuhusu uongozi na namna ya kuongoza nchi.

Aliongeza kuwa katika matusi yake alimtuhumu Mke wa Raisi kuwa ni Mwanamke Mpumbavu anayeibomoa nchi nyumba yake kwa mikono yake Mwenyewe kama Biblia inavyosema na kwamba yeye atakuwa tayari kumshauri Dk. Slaa atakapokuwa Raisi mwaka 2015.


Kutokana na tuhuma hizo Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya wamemtaka Mke wa Dk. Slaa kuacha tabia ya kumsema vibaya Mama Salma na akiendelea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha na Mbeya yetu

2 comments:

Anonymous said...

Pembe za ndovu na ile mseme nan atafuata kung'olewa kucha na meno
mwigulu nchemba

Anonymous said...

Mbona sijaona la maana zaidi nanyi kutaka kujipendekeza ili Mh Rais awajue nyie ni akina nani bt ukweli hamna hoja ya msingi hapo. lkin kingine inaonesha ata upeo wa viongozi hauna mambo mengine ya kuzungumza zaidi ya kuja ma mabishano ambayo kwetu sisi hayatusaidi hata kidogo. Jipangeni upya kuna mengi mnayo sema hamjui km yanatakiwa kufanyika au mmemezwa na mfumo