Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 13, 2013

LIGI YA MWAKISU CUP YAZINDULIWA JIJINI MBEYA

Vijana wa jijini Mbeya wapenda michezo wakiandamana kuelekea kwenye uzinduzi wa ligi ya Mwakisu Cup

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki.  akisalimiana na Refalii Bitebo kabla ya uzinduzi 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki. akizindua mashindano ya Mwakisu cup. 
Masaki alisema njia kuuu ya Vijana kuondokana na uhalifu ni pamoja na kushiriki michezo ambayo huwakutanisha pamoja hivyo kukosa muda wa kufikiri vitendoviovyu ambavyo havina maslahi kwa taifa na kuongeza kuwa Michezo ni afya hivyo ni jukumu la kila kijana kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika Michezo.

 Mdhamini mkuu wa ligi hiyo ya Mwakisu Cup, Nwaka Mwakisu amesema ndoto yake kubwa katika maisha ni kuona vijana hawakosi kazi ya kufanya na ndiyo maana kajitolea kuanzisha ligi ambayo itawafanya vijana wote bila kujali itikadi za kisiasa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na kushabikia na kushiriki.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki. akipiga penati kuashiria uzinduzi wa Mwakisu Cup
Aidha pamoja na mvua kubwa kunyesha mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha timu za Airport Rangers Fc na Terminal Fc uliendelea hivyo hivyo kutokana na uwanja uliotumika kutotunza maji hivyo kutokuwa sababu ya kuahirisha mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi wa kati Bitebo Manduta.


UFUNGUZI wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya Kombe la Mwakisu nusura uingie doa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana mara tu baada ya mgeni rasmi kutangaza kuyafungua mashindano hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbata Jijini Mbeya.

Mvua hiyo ilianza majira ya saa kumi na nusu jioni ilileta hofu kwa maelfu ya mashabiki waliofurika katika viwanja hivyo kushuhudia mechi za ufunguzi katika Ligi iliyozinduliwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki.

Masaki alisema njia kuuu ya Vijana kuondokana na uhalifu ni pamoja na kushiriki michezo ambayo huwakutanisha pamoja hivyo kukosa muda wa kufikiri vitendo viovu ambavyo havina maslahi kwa taifa na kuongeza kuwa Michezo ni afya hivyo ni jukumu la kila kijana kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika Michezo.

Kwa upande wake mdhamini mkuu wa ligi hiyo ya Mwakisu Cup, Nwaka Mwakisu alisema ndoto yake kubwa katika maisha ni kuona vijana hawakosi kazi ya kufanya na ndiyo maana kajitolea kuanzisha ligi ambayo itawafanya vijana wote bila kujali itikadi za kisiasa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na kushabikia na kushiriki.

Mwakisu alizitaja zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa Michuano hiyo yenye timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne kuwa ni Mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Fedha taslimu shilingi Milioni 2,Msindi wa Pili Milioni 1 na Mshindi wa tatu ikiibuka na Shilingi Laki tano tu.

Aidha pamoja na mvua kubwa kunyesha mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha timu za Airport Rangers Fc na Terminal Fc uliendelea hivyo hivyo kutokana na uwanja uliotumika kutotunza maji hivyo kutokuwa sababu ya kuahirisha mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi wa kati Bitebo Manduta.

Katika mchezo huo timu ya Terminal Fc ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa Magoli 2 kwa Moja dhidi ya timu ya Airport  Rangers, hata hivyo timu ya Airport ilibidi ijilaumu yenyewe kutokana na kukosa magoli mengi katika kipindi cha kwanza baada ya kujipatia goli la kuongoza dakika ya kumi ya mchezo kupitia kwa mchezaji wake Amoni Sanga.

Timu ya Terminal ilifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 45 kabla ya mapumziko ambapo timu zilienda mapumzikoni zikiwa sare ya kutoshana nguvu kwa goli moja moja, kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu zikishambuliana kwa zamu na kuwaweka katika hali ngumu Walinda milango kufuatia mpira kuteleza mikononi kutokana na mvua kubwa lakini Terminal walifanikiwa kufunga goli la pili na ushundi dakika ya 40 ya kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wake Issa Nelson.
  
Kwa upande wake mratibu wa ligi hiyo David Mwakalinga  alisema ratiba maalumu ya ligi hiyo haijapangwa vizuri kutokana na baadhi ya timu kusuasua kujiandikisha ambapo alizitaja baadhi ya timu zilizothibitisha kushiriki michuano hiyo kuwa ni Airport, Terminal, Zaragoza, Ghana, Temeke, Maji ya Ugoko, Jangwani, Uhindini, Nyota, Black Eagle, Simike, Inter Forest, Saitama na Majengo.

Picha na Mbeya yetu 
 

No comments: