Gari aina ya scania yenye nambali za usajiri T578 ALS likiwa na tela nambli T125 AGM lililobomoa nyumba na kusababisha vifo vya watu 3 wa familia moja |
Wananchi wa kijiji cha Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakiwa msibani |
WATU
watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari
aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
Tukio
hilo lilitokea jana majira ya saa Tatu na Robo usiku katika Kijiji cha Ilongo
Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari kugongana na
kugonga nyumba na kusababisha vifo na majeruhi.
Alisema
chanzo cha ajali kilitokana na Gari lenye namba za usajili T578 ALS likiwa na
tela lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania likiendeshwa na dereva
ambaye hakuweza kutambulika liligonga kwa nyuma gari lenye namba
T959 ASC aina ya Scania.
Alisema
gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Juhudi Saimon(34)Mnyiha mkazi wa Dar
Es Salaam kisha gari hilo kugonga nyumba mali ya Matia Mwagala
mkazi wa Kijiji cha Ilongo.
Aliwataja
matrehemu kuwa ni Asia Yahaya (52)mkulima na Msangu, Abubakari Yahaya(8) Msangu
na mwanafunzi darasa la pili aliyekuwa anasoma katika Shule ya msingi
Ilongo na Fatuma Yahaya (6) Msangu mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule
ya Msingi Ilongo wote wakazi wa kijiji hicho.
Aidha
aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na Abuu Fadhil (22)Mzigua
mkazi wa Dar Es Salaam ambaye ni tingo wa gari lililogonga Nyumba pamoja na
Steven Chiwa (26) mbembe raia na mkazi wa Nchi jirani ya Zambia ambaye ni
msindikizaji wa gari hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya
Chimala.
Hata
hivyo wa dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara baada ya
tukio ambapo Kaimu Kamanda anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya
mahalialipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo azitoe katika mamlaka
husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo ajisalimishe mara
moja.
Wakati huo huo
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Asajile Mwamtina (46) mkazi
wa kijiji cha Syukula Wilaya ya Rungwe mkoani hapa akituhumiwa kufanya mapenzi
na binti yake wa miaka 13.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
lilitokea juzi majira ya saa Kumi na Mbili jioni baada ya kumvizia binti
huyo (jina limehifadhiwa) ambaye aliacha shule akiwa darasa la tano mwaka 2011
kwa matatizo ya ugonjwa wa kifafa akiwa anapika.
Alisema mtuhumiwa
alipata mwanya wa kufanya unyama huo kutokana na mkewe ambaye mama
mzazi wa mhanga huyo Tumikigwe Samalinga akiwa kijiji cha Kiwira
kuuguza mgonjwa na kuongeza kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika.
Aidha
katika tukio lingine eneo la Makunguru Jijini Mbeya Vyumba 12 vya biasharaa
viliteketea kwa moto jana majira ya saa Tano asubuhi vilivyokuwa vimetoka
kujengwa mali ya Dominick Mbinga Mkazi wa Dar Es Salaam.
Hata
hivyo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza baada ya moto huo kudhibitiwa
kwa ushirikiano baina ya kikosi cha zima moto na uokoaji na wananchi.
Thamani halisi ya uhalibifu bado kujulikana
pamoja na chanzo ingawa kwa mujibu wa majirani walisema inawezekana ikawa ni
hitilafu ya umeme kutokana na muda huo wapangaji wa nyumba hiyo kutokuwepo
wakati moto ukitokea ambao ulijulikana baada ya majirani kuona.
No comments:
Post a Comment