MNAMO TAREHE 17/03/2013 MAJIRA YA
SAA 21:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGAWA BARABARA YA MBEYA /IRINGA WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI NO T. 405 AJQ AINA YA SCANIA EASY BUS LIKIENDESHWA
NA DEREVA AJALI S/O MOHAMED, MIAKA 32, MHEHE, MKAZI WA IRINGA LIKITOKEA NCHINI
MALAWI KWENDA DSM LILIACHA NJIA NA
KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO
VYA ABIRIA SITA [06] NA MAJERUHI 25 . ABIRIA WALIOFARIKI WATANO NI RAIA WA
NCHINI MALAWI WALIOTAMBULIWA KUWA NI 1.ASAM
S/O MKAZI WA WILAYA YA BARAKA 2.
BONZO S/O ? 3. ADAM S/O SAKWATI MKAZI WA BLANTYRE NA 4. MARIA D/O ? MKAZI WA ZINGWANGWA- BLANTYRE 5. MTOTO MDOGO JINSIA KIKE UMRI MWAKA MMOJA NA 6 RAJABU S/O HASSAN,MIAKA 35,MSAMBAA KONDAKTA WA BASI HILO AMBAYE
ALIFARIKI WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA ILEMBULA . MIILI YA MAREHEMU WATANO
IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MAJERUHI 25 KATI YAO 14 WANAUME
NA WANAWAKE 11 WAMEPELEKWA HOSPITALI YA MISHENI ILEMBULA KWA MATIBABU. CHANZO
NI UZEMBE WA DEREVA WA BASI T. 491
BBJ AINA YA NISSAN KAMPUNI YA TAQWA AITWAE KENETH S/O THOMAS,MIAKA 48,MKAZI WA
KABWE-MBEYA WAKATI AKIJARIBU
KULIPITA BASI T405 AJQ NA KUKUTANA
NA GARI LINGINE MBELE YAKE KISHA
KUAMUA KURUDI GHAFLA NDIPO BASI LA NYUMA YAKE KUPOTEZA UELEKEO NA KUACHA NJIA .
DEREVA KENETH S/O THOMAS AMEKAMATWA NA DEREVA AJALI S/O MOHAMED ALIKIMBIA MARA
BAADA YA TUKIO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed By,
[ DIWANI ATHUMANI-ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment