CHAMA cha watu wenye ulemavu (CHAWATA) mkoani Mbeya
kimependekeza katiba ijayo iruhusu wawakilishi wa walemavu katika ngazi ya
halmashauri na bunge wapatikane kwa kupigiwa kura. Mapendekezo hayo yametolewa na wajumbe waliohudhuria mdahalo
wa kuwajengea uwezo walemavu kuchambua katiba ya nchi ya sasa na kuibua
mapendekezo ya kuingizwa kwenye katiba mpya uliofanyika katika ofisi za chama
hicho jijini hapa kwa ufadhili wa shirika la The Foundation For Civil Society.
Mmoja wa wajumbe hao Willium Simwali kutoka wilayani Mbeya amesema mfumo uliopo
sasa wa rais kuteua mwakilishi wa jamii ya walemavu bungeni hautoi demokrasia
badala yake mwakilishi huyo alipaswa kupatikana kwa kupigiwa kura. Simwali
amesema vyama vya watu walio na ulemavu ndivyo vinapaswa kushiriki mchakato wa
kutafuta mwakilishi kuanzia katika ngazi za mitaa kwa kila kimojawapo kutoa
mgombea na kumshindanisha na vyama vingine vya watu wa jamii hiyo. Naye Isaya
Kyando kutoka Mbozi ametaka katiba ijayo itoe maelekezo ya vifaa kwaajili ya
walemavu kuuzwa kwa bei zitakazowawezesha kumudu kununua na pia serikali kuwa
na fungu kwaajuili ya kuwawezesha watu wa jamii hiyo hususani kwa kuwanunulia
vyombo vya usafiri. Mwenyekiti wa Chawata mkoani hapa Jimmy Ambilikile amesema
mdahalo huo umehudhuliwa na wajumbe wawakilishi kutoka wilaya zote za mkoani
hapa ambao licha ya kutoa maoni yao pia watapeleka mrejesho wa wanachama
watakaporejea wilayani kwao
Kwa hisani ya Joachim Nyambo
No comments:
Post a Comment