WANAUSALAMA WAKIONDOKA KATIKA MKUTANO ULIOVUNJIKA
MKUU WA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA
DR. MICHAEL KADEGE
AMEJIKUTA KWENYE HALI NGUMU BAADA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA MLOWO
KUMZOMEA NA KUVURUGA MKUTANO WA KIJIJI AMBAO ULIKUWA NA MADHUMUNI YA KUTATUA MGOGORO ULIODUMU KWA MWAKA
MMOJA BAINA YA KIJIJI HICHO NA HALMASHAURI YA WILAYA KUHUSIANA NA MAKUSANYO YA
USHURU KWA WAFANYA BIASHARA.
AIDHA WANANCHI HAO WAMEPINGA KITENDO CHA MKUU WA WILAYA
KUMSIMAMISHA MWENYEKITI WA KIJIJI BWANA DAUD KATULE KWA TUHUMA ZA UBADHILIFU WA
FEDHA ZA KIJIJI , KUTOSOMA MAPATO NA MATUMIZI PIA KUCHAPISHA VITABU VYA
KUKUSANYA PESA NA KUTOWASILISHA FEDHA KATIKA OFISI YA ALMASHAURI.
KADEGE AMESEMA SABABU HIZO NDIZO ZILIMPELEKEA KUMSIMAMISHA
UONGOZI BWANA KATULE NA KWAMBA ALIITWA KWENYE KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA
MAPINDUZI NA HALMASHAURI YA WILAYA
AMBAPO IMEDAIWA KUWA ALIKIRI KUFUJA PESA HIZO NA KUAHIDI ATAZIREJESHA
LAKINI HAKUTEKELEZA HALI ILIYPOLEKEA KUSIMAMISHWA UONGOZI TANGU JANUARI 2013.
KUFUATIA MVUTANO HUO WANANCHI WALIFUNGA OFISI YA KIJIJI
MWANZONI MWA WIKI HII KUSHINIKIZA SERIKALI KUTATUA MGOGORO HUO.
MKUU WA WILAYA AMEAGIZA OFISI IFUNGULIWE MARA MOJA ILI
SHUGHULI ZA SERIKALI ZIENDELEE KAMA KAWAIDA AMBAPO OFISI ILIFUNGULIWA SAA 10.
00 CHINI YA MTENDAJI KATA JACKSON MWANA NA MTENDAJI KIJIJI JUDHITH MTEGA.
HATA HIVYO MKUTANO HUO ULIDHIBITIWA NA JESHI LA POLISI KWA
KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA AMBAPO WANANCHI WAMEBAKI
HEWANI KWA KUSHINDWA KUTATULIWA MGOGORO HUO.
Na kamanga Mbeya
|
No comments:
Post a Comment