MNAMO TAREHE 12.02.2013 MAJIRA YA SAA
11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA
S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA
BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NDANI YA NYUMBA YAKE .
MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA KIUNGO
HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA ANAKIRI
KUMILIKI KIUNGO HICHO AMBACHO ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA
KIENYEJI KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA
KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE
KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA NA FEDHA ZAKE.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA
POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA
KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO
KWA BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO.
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA
KUUCHUKIA UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA
UNAOJITOKEZA KATIKA MAENEO YAO.
Signed by
[B.N.MASAKI -SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MBEYA
|
No comments:
Post a Comment