Mkuu wa
Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela. akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mpira kwisha
Timu ya
Mbeya City inayocheza Ligi daraja la kwanza Tanzania bara, imejiweka kwenye
nafasi nzuri ya kupanda daraja kwa kushiriki ligi kuu msimu ujao baada ya
kuichapa timu ya Polisi Iringa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja
wa Sokoine mjini Mbeya.
Katika
msimamo wa ligi daraja la Kwanza timu ya Mbeya City ina Pointi 22 na ndiyo
inayoongoza kundi A ikifuatiwa na Polisi Iringa iliyo na Pointi 14, hivyo Mbeya
City ikishinda mechi mbili kati ya nne zilizobaki itashiriki ligi kuu msimu
ujao
Na mbeya yetu.
|
No comments:
Post a Comment