Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini
MAHAKAMA ya Wilaya ya
Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Wilvina Mkandara(24) kutokana na kesi
iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto wa shemeji
yake.
Akisoma hukumu hiyo
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alisema mshakiwa amehukumiwa
kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.
Amesema Mahakama
inaweza kumtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira au ushahidi
wa moja kwa moja ambapo alisema mshtakiwa anahukumiwa kutokana na ushahidi wa
mazingira kwa sababu mhangwa wa tukio hilo alishindwa kutoa ushahidi wa moja
kwa moja.
Ameongeza kuwa
mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo
kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto ili hali alikuwa mama mlezi ikiwa ni
pamoja na kumpeleka Hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.
Ndeuruo amesema pia
mahakama hiyo haikuridhishwa na na ushahidi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani
kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mhanga wa tukio hilo yalitokana na kuugua
kwa tetekuwanga jambo ambalo alisema si la kweli.
Amesema kuwa mshtakiwa
ametoa maelezo wakati wa utetezi wake yanayopingana na na maelezoya daktari
aliyemtibu mgonjwa alipofikishwa hospitali wakati akitoa ushahidi mahakamani
hapo.
Hata hivyo kabla ya
kutoa hukumu hiyo Hakimu huyo alisema kutokana na ibara ya 16 ya sheria ya African
Charter inayotaka Nchi itunge sheria ya kulinda haki za watoto ambapo Tanzania
haina sheria hiyo hivyo kusababisha watu kuwanyanyasa watoto.
Hakimu huyo ametoa
wito kwa taasisi zinazohusika kutunga sheria hiyo mara moja ili kulinda haki za
watoto ambayo itatamka wazi adhabu kwa wale watakaobainika kuwatesa na
kuwanyanyasa watoto.
Kwa upande wake
mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa ameiiambia mahakama hiyo kumpa
adhabu kali mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia
kama hizo ambao hajakamatwa.
Amesema kitendo
kilichofanya na mshtakiwa huyo ni kitendo chakinyama ambacho kinatakiwa
kulaaniwa vikali hivyo kupitia adhabu atakayopewa mtuhumiwa inaweza kupunguza
unyasasaji kama huyo katika jamii.
Aidha mshtakiwa Wilvina
alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa aliomba mahakama
hiyo impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa ni mjamzito, pia hajui mtoto
wake aliyemzaa alipo pamoja na mawasiliano na familia yake.
Akitoa hukumu hiyo
hakimu Ndauruo amesema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa cha kuomba
kupunguziwa adhabu kutokana nakutomwona mtoto wake hali inayoonesha kutomjali
mtoto aliyemtendea kosa.
Ameongeza kuwa
Mahakama imefuatilia historia ya nyuma ya mtuhumiwa ambayo haioneshi kama
anamatukio kama hayo ambayo aliwahi kuyafanya lakini mtuhumiwa anastahili
adhabu kali kama upande wa mashtaka ulivyo sahauri na kutokana na mhanga kuwa
na ulemavu wa kudumu.
Amesema mahakama
inamhukumu kifungo cha maisha kifungo kitakachothibitishwa na mahakama kuu
kutokana na mtuhumiwa kuwa na haki ya kukata rufaa kama ameona ameonewa katika
kesi hiyo.
Mwanamke huyo
alipandishwa kizimbani Novemba 16, Mwaka chini ya Mwendesha mashtaka wa
Serikali, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala
(24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo
imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.
2 comments:
Yaani binadamu ni kama chui,mtoto anafanyiwa mabaya na hana hata nguvu za kujitetea masikini lakini bado roho yako haiingiwi na imani ya kimungu ili ujione kuwa unayotenda si mazuri?looh nenda dada gerezani ukaishi maisha yako yote kwani hufai kuishi kwenye jamii yetu,tena nakwambia laana i juu yako kwa chozi lililodondoka kwa mtoto Aneth ulipokuw unamtesa
pongezi kwake hakimu safi sana tena angempa na adhabu ya mateso kama alivyomtesa huyo mtoto
Post a Comment