Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, February 1, 2013

BAADHI YA WANANCHI WANANCHI MBEYA WALALAMIKIA MAKAMPUNI YA VINYWAJI BARIDI KUTOWAJALI AFYA ZAO

HII NI AINA YA SODA  TONIC WATER YA KAMPUNI YA COCA COLA  MBEYA IKIWA NA KILOBA CHA POMBE KALI AINA YA VODKA


WANYWAJI WA VINYWAJI BARIDI  MNAONA HIYOOO



BAADHI ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi Jijini Mbeya wameyalalamikia baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji wa bidhaa hizo kwa kutozingatia usalama wa watumiaji.

Malalamiko hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina lake kununua soda aina ya Tonic Water inayotengenezwa na kampuni ya Coka kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina ya Vodka.

Soda hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka moja eneo la Simike baada ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini kabla ya kuifungua ndipo laipogundua uchafu huo.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa stori hii  alipewa taarifa na mhusika ambapo walienda moja kwa moja hadi kiwandani Coka eneo la Iyunga Jijini Mbeya na kupokelea na Meneja mauzo wa wilaya(Area sales Manager)

Baada ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea meneja huyo aliwapeleka waandishi kwa kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema tuwaachie soda hiyo baada ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.

Walidai waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa kimaabara katika uchunguzi utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta sintofaham kwa walalamikaji huku wakihoji uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu unaonekana.

Aidha walidaikuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda hiyo walisema mlalamikaji hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika na tatizo hilo licha ya kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.

Hali kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji hivyo hasa wanaotumia  nyakati za usiku muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika vinywaji.

Hata hivyo mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka kiwanda cha Coka aliiomba mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea vinywaji hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili kunusuru afya za wananchi.


No comments: