Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, January 28, 2013

SHITAMBALA KUONGOZA MAANDAMANO WANANCHI 5000 KUMVAA KANDORO KUPINGA KUHAMISHWA

MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa  Bw.Sambwee Sitambala



,asema  yatakuwa ya amani bila  Vurugu
,asema  sera ya  CCM ni kutetea  wananchi
MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa  Bw.Sambwee Sitambala  anatarajiwa kuongoza  maandamano  ya amani  ya wananchi  zaidi ya  5000 wa  mtaa  wa Gombe  kusini  kwenda  kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kupinga amri ya kutaka  kuwahamisha  kwenye  nyumba zao na eneo hilo kupewa  watu wengine.

Akizungumza   na waandishi wa habari baada ya kwisha  kwa mkutano wa wananchi hao diwani wa Kata ya  Itezi  jijini Mbeya  Bw.Frank Mayemba ambaye  pia ni mjumbe wa Mkutano  mkuu Taifa  CCM alisema kuwa  katika  maandamano hayo  watashirikiana  na  Bw.Shitambala  kuongoza   hadi kufika kwa mkuu wa Mkoa.

Alisema kuwa wananchi hao ambao zaidi ya asilimia  90 ni wanachama wa CCM walifikia  hatua hiyo baada ya kuona  hawasikilizwi  katika kilio chao ambacho wamekuwa wakitoa kwa Jiji la Mbeya kuwataka kutowagusa kwa kuwa walipewa maeneo hao kihalali baada ya kubadilishwa  matumizi yake  ya awali ambayo yalikuwa viwanda.

Bw.Mayemba alisema kuwa  kutokana na hali hiyo wamedhamiria  kudai haki yao kwa mkuu wa Mkoa ambaye  ndiye msimamizi wa Halmashauri zote Mkoa wa Mbeya  ambapo kutokana na hekima  yake  walisema kuwa wana imani kuwa atawasaidia kuwasikiliza  ombi lao na kusitisha  zoezi hilo ambalo ni  athari kubwa kwa wananchi hao.

Alisema kuwa  wananchi hao baada ya kupewa viwanja hivyo  wamekaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka  20 na hivyo kisheria kuwa  wamiliki haklali wa  maeneo haio wasio takiwa kubughudhiwa  na hivyo kushangaa wakati wote wanapoambiwa kuwa watahamishwa na  maeneo yao kupewa  watu wengine.

"sisi tunasema    kama viongozi wa chama   hakika hatutakubali  suala  hili kwa kuwa ni wamiliki  halali wa eneo hili  na hivyo kama wanataka kugawa  basi tuweke mkataba ambao  watatugawia  sisi na wala si wengine  kama wanavyotaka kufanya  sasa  hawa  wataalam."alisema.

Naye  Bw.Shitambala ambaye pia  ni Kaptain wa jeshi mstaafu na mwanasheria  maarufu alisema kuwa  ataongoza  maandamano hayo ya amani hadi kwa mkuu wa Mkoa   na hakuna vurugu itakayotokea  kwa kuwa  CCM ni chama kinachohamasisha  amani na utulivu na  hivyo wao wataonesha  mfano.

Kada huyo wa CCM ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla   ya kumamia  chama hicho alisema kuwa wataomba vibali polisi kwa ajili ya kulinda maandamano  hayo na kamwe hawatachoma  barabara kama wanavyofanya  wengine  ambnapo watapata nafasi ya kumweleza  mkuu wa Mkoa   hoja  zao zinazopinga  kuondolewa katika  eneo hilo .

Alisema   yeye kama  mkazi aliyejenga  eneo hilo ni dhambi kubwa kuona  wananchi wenzake na yeye akiwemo wakinyanyaswa   na hivyo kupelekea  hasira kali kwa chama  hali ambayo alisema kuwa katika  mkutano mkuu wa chama  na  vikao mbali mbali wamekubaliana kupinga  hali hiyo  na kuwapa haki yao wanachama .

Kwahisani ya Charles Mwakipesile Mbeya

No comments: