HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imeshauriwa kumaliza mgogoro kati
yake na wakazi wa eneo la Sokomatola kwa kuruhusu wakazi hao kufanya mazungumzo
na wafanyabiashara wakubwa wao wenyewe ili waweze kukubaliana na kuuziana
nyumba.
Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa ikilumbana na wakazi wa eneo
hilo ambapo ilitaka kuwahamisha na kisha ichukue ilichukue na kugawa viwanja upya
kwa watu walio na uwezo wa kujenga maghorofa lengo likiwa ni kupendezesha mji.
Hali hiyo inatokana na nyumba nyingi zilizopo katika eneo la Sokomatola kuwa za
kizamani na zilizochakaa hali isiyoendana na madhari ya kisasa yaliyopo kwenye
kituo cha mikutano cha Mkapa cha halmashauri ya jiji la Mbeya kilichopo maeneo
hayo. Lakini Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameshauri halmashauri
kuwaruhusu wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kufanya maamuzi wao wenyewe kwa
kukubaliana na watu walio na uwezo wa kujenga magorofa na si kuwaingilia.
“Tumeona mahala kwingi wafanyabiashara au wawekezaji wakubwa wanawafuata watu
walio na viwanja na kufanya mazungumzo nao na wanakubaliana vizuri.Wengine
wanawajengea nyumba mbali kisha wanawaachia viwanja ama wanakubaliana ikijengwa
ghorofa huyu amiliki vyumba kadhaa na mwenzake vinavyobaki”. “Halmashauri
isiingilie makazi ya watu.Mnadumaza eneo la Sokomatola.Na mnatudanganya kusema
ninyi mtalinunua kasha muuze viwanja upya pesa hamna mtazitoa wapi.” Kandoro
pia alishauri halmashauri kufanya mazungumzo na kituo cha utafiti wa kilimo cha
Uyole jijini hapa ili ili iweze kupewa eneo la mbele lililo pembezoni mwa
barabara ili litumike kwa ujenzi wa makazi badala ya kilimo kama linavyotumika
hivi sasa. Alisema ili kuwa na mji wenye mwonekano mzuri ni vema halmashauri
ikajipanga na kuhakikisha hakuna vichaka katikati ya mji badala yake iwezeshe
wakazi kupata viwanja kwenye maeneo yaliyo wazi na kujenga
|
1 comment:
Halmashauri yetu ya Mbeya!
Tunaamini wana lengo zuri la kuwasaidi wananchi wa SokoMatola, tunachoomba ni kuwa muelekeo usiwe kuwafanya wahisi tofauti. Napenda kuongeza kwenye maneno ya Mheshimiwa mkuu wa mkoa kuwa, pengine kwa kuwaunganisha wananchi haoa na shirka la nyumba (NHC) wanaweza kupata manufaa zaidi kwani shirika hilo linashughulikia kujenga, na kupangisha,hivyo wanaweza kumpatiia mwananchi nyumba mahali pengine ,na kumpatia baadhi ya vyumba akawa anapata pesa ya kuendelea kuendesha maisha yake siku za usoni! Kama Halmashauri itakuwa kwenye mtazamo wa jinsi hii,naamini wananchi watato ushirikiano!
Post a Comment