KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo vya
rushwa katika taasisi za Serikali, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya imeamua kuandaa
Bonanza kubwa la michezo kwa ajili ya kukutana na wananchi ili kukemea vitendo hivyo.
Aidha hali hiyo imekuja ikiwa ni siku
chache baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kuingiwa na kashfa kwa baadhi ya
watumishi wake wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya Kupokea Rushwa kutoka
kwa wagonjwa hususani katika kitengo cha Mifupa.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, katibu wa Hospitali hiyo, Aisha
Mtanda alisema kuwa bonanza hilo ambalo litabeba ujumbe usemao ‘Huduma
bora bila rushwa inawezekana, kemea vitendo vya vya rushwa, tuungane
kutokemeza limeandaliwa na Uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na
kampuni ya LifeTime Entertainment & Marketing Ltd na kwamba bonanza hili
litafanyika siku ya Jumamosi(Januari 26, mawaka huu).
Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni
kufanya hafla fupi kwa watumsihi wa Hospitali hiyo kwa kuaga mwaka wa 2012 na
kuukalibisha mwaka mpya wa 2013, ambalo pia litafanyikia katika viwanja vya
Chuo cha Uhasibu (TIA)tawi la Mbeya.
“Uongozi wa Hospitali tunakusudia
kufanya bonanza litakalowakutanisha watumishi wa serikali pamoja na taasisi
mbalimbali siku ya Jumamosi Katika bonanza letu litakuwa na ujumbe wa kukemea
vitendo vya rushwa vinavyoonekana kushamiri katika sekta mbalimbali,” alisema
katibu huyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza
hilo kutoka Kampuni ya Lifetime Venance Matinya alisema katika Bonanza hilo
kutakuwa na michezo mbali mbali kama vile mpia wa miguu, mpira wa pete,
Netboli, Basketi boli, Voleboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia,kukuna
nazi na mashindano ya kula.
Aliongeza kuwa taasisi zinazotarajia
kushiriki ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Halmashauri ya Jiji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Madiwani wa Halmashauri wa Jiji, Kampuni ya Bia
(TBL), Hospitali ya Rufaa na kitengo cha Benki ya damu salama.
Naye meneja wa kampuni hiyo ya
LifeTime Entertainment, Emmanuel Madafa, alisema kuwa katika mabonanza hayo ni
sehemu pekee ya kukutana kwa watumishi mbalimbali na wananchi ili kuweza
kuambizana ukweli kuhusu adii mbaya wa rushwa.
Alisema kuwa vitendo vya rushwa
haviwezi kukomeshwa endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa kuambizana
ukweli, kwani wananchi muda mwingine wanaweza wakawa wanashawishiwa kutoa
rushwa kutoka kwa watumishi bila ya kujua haki zao za msingi na wasijue wapi
wanaweza kwenda kutoa malalamiko yao.
“kwenye mabonanza kama haya ni sehemu
pekee ya kuweza kukutana wananchi pamoja na watumishi wa Serikali na taasisi
mbalimbali ili kuweza kuambizana ukweli kuhusu adui rushwa kwani hawa watu
wawili ndiyo wahusika wakuu kwamaana ya mpkeaji na mtoaji,” alisema Madafa.
Hivi karibuni Mmoja wa watumishi wa
Hospitali hiyo wa kitengo cha mifupa alikamatwa na taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU) na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea
rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa anahitaji kupatiwa huduma ya upasauaji.
|
No comments:
Post a Comment