Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 17, 2012

ALIYEDHANIWA AMEKUFA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JUMAMOSI AFUNGA NDOA HAKIKA MUNGU NI MKUU

Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth  Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya
Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100  Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo 
Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo  katika kanisa la agape 
Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani
Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa
Sasa bana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa
Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete  huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea
Hapa wakipata mibaraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE
Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota

Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa
Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao
Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya ccm jijini mbeya
Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo ingawa maharusi hawakuweza fika kwenye sherehe hiyo kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu



Picha na Gwasa wa Mbeya yetu

4 comments:

Anonymous said...

jamani hili ndo penz la kweli na mungu atawajaalia watakuwa pamoja wote daima inshaallah..bi harusi anaonekana kabisa anafuraha ya kuoana na mwenzie wangekuwa wengine hapo wangejitia,ooh harusi iahirishwee,lol..GOOD JOB.bi harusii mungu akuzidie moyo wa huruma zaidi na zaidiii

Anonymous said...

God is Great

Anonymous said...

mwacheni mungu aitwe mungu....!!! kwa jinsi picha ya ajali ilivyo, ni mkono wa mungu tu uliomuepusha bwana harusi na kifo, hakika Yehova you are faithfully.... Binadamu tunatakiwa tuwe na hofu ya mungu na tutembee kwa uwepo wa mungu kila saa kwa sababu hatujui siku wala saa
Praiseeeeee the Lord....!!!

Anonymous said...

Kweli Mungu yu mwema jamaniiii