MNAMO TAREHE 31.10.2012
MAJIRA YA SAA 18:45HRS HUKO ENEO LA SAE MBILINYI JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI
T.545 AZE SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA ABOOD ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA
MUSSA S/O KILASI, MKAZI WA DAR ES SALAAM ILIGONGANA NA GARI T.610 ATQ/T253 APL
SCANIA LORY ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA MARA
MOJA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHARLES S/O KITELEKE, MIAKA 42, KONDAKTA WA BUS LA
ABOOD MKAZI WA MOROGORO WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO
WATU 23 WALIJERUHIWA KATI YAO 15 WALIPATA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA MAJERUHI 8
WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KATI YAO WANAUME NI 5 NA WANAWAKE NI 3 NA
HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
MAJERUHI WALIOLAZWA NI 1.
NICUS S/O KAYUNI, MFIPA, 45, MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 2. ANDREAS S/O MBILA,
MKINGA, 32YRS, MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 3. ZAMOYONI S/O WATSON, 28YRS, MSAFWA,
MFANYABIASHARA WA TUNDUMA 4. VUMILIA S/O MWAZEMBE, MNYIHA, 31YRS, MKAZI WA
MPEMBA 5. ALINAMAKA S/O MAHENGE 6. ANKA D/O MYAMBO, 45YRS, MZAMBIA 7. HILDA D/O
CHILWA, 40 YRS, MKAZI WA ZAMBIA 8. GIFT D/O NANKALA, 40YRS, MKAZI WA MAMBWE
ZAMBIA.
CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI WA GARI T.610 ATQ/T.253 APL SCANIA AMBALO LILIKUWA LINAJARIBU
KUPITA GARI JINGINE NA KWENDA KUGONGANA NA BASI HILO.
MADEREVA WA MAGARI YOTE
MAWILI WAMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA MAGARI HAYO BADO YAPO ENEO LA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI NA VYOMBO VYA USAFIRI NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAI KWA
MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIKO MADEREVA HAO AZITOE KWA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[ DIWANI ATHUMANI –
ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment