|
Mbunge wa Mbozi Mashariki na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya GODFREY ZAMBI akimkaribisha Mkuu wa mkoa ABASI
KADORO jimboni kwake kwa ajili ya Ufunguzi wa ofisi ya kisasa ya kata ya
Mlangali.
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO
akivishwa Skafu na skauti wa kata ya Mlangali wilayani Mbozi kabla ya kufungua
jengo jipya la ofisi ya kata hiyo.
|
|
Mkuu wa wilaya ya Mbozi DKT.MICHAEL
Y.KADEGHE akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa ABASI KANDORO kabla ya kufungua jengo
hilo
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akifungua Ofisi ya kata ya Mlangali iliyogharim zaidi ya shilingi Milioni 38 |
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akimuonesha Mbunge wa
jimbo hilo Madhaifu ya fundi wa jengo hilo, ambapo alisikitishwa na kitendo cha
Mlango wa Mninga kupakwa rangi ikiwa ni pamoja na mbao za mlango huo kutobanwa
vizuri hali inayopelekea kuwepo kwa matobo mlangoni
|
|
Mkuu wa mkoa ABASI KANDORO akimtaka
fundi wa jengo hilo kutoa sababu ya kupaka rangi mbao za mininga ikiwa ni
pamoja na kupaka ripu dirisha, hata hivyo alimtaka fundi kuhakikisha ripu hiyo
inaondolewa kwenye ubao na kuhakikisha ubao unapigwa msasa ili kuonesha
uhalisia wa mbao iliyopo.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO
akipanda Mti mbele ya ofisi hizo kwa lengo la kuhamsisha jamii utunzaji wa
mazingira.
|
|
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi na Momba LEVISON CHILEWA akipanda naye mt
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dkt.MICHAEL Y.KADEGHE akipanda mt
|
|
Mbunge wa Mbozi Mashariki na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya GODFREY ZAMBI akipanda mti mbele ya ofisi za
kata ya Mlangal
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO
akicheza ngoma ya kinyakyusa baada wachezaji wa ngoma hiyo ambao wengi wao ni
wazee wakicheza kwa ustadi hali iliyomlazimu kunyenyuka kwenye kiti na kwenda
kujiunga nao
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akabidhiwa uchifu
Mbozi,huku machifu hao wakitoa onyo kwa mtu atakaye jaribu kupuza maagizo ya
chifu huyo mpya ndani ya Mbozi na mkoa kwa ujumla
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO
akihutubia maelfu ya watu wa tarafa ya Iyula ambao walihudhuria ufunguzi wa
ofisi ya kata ya Mlangali.
Katika Hotuba yake Kandoro alisistiza
Umoja na mshikamo, utii wa sheria bila shuruti, ushirikiano katika kuendeleza
na kukuza shughuli za kimaendeleo, pembejeo za kilimo ambapo aliwataka wakulima
kutokubali kurubuniwa na mawakala wadanganyifu kwa kurubuniwa kupewa pesa
badala ya mbolea.
Hata hivyo amesema kuwa Ruzuku
itatolewa kwa mbolea ya Minjingu na sio vinginevyo.
Kuhusu mabaraza ya kata Kandoro ataka
faini isizidi elfu 10 na kuwepo kwa haki bila upendeleo huku rufaa ya watu
kwenda mahakamani zitolewe kwa haki.
|
Habari kwa hisani ya Bwille Media Mbeya
No comments:
Post a Comment