MGOGORO uliozuka kati ya mkandarasi wa soko la Mwanjelwa
linaloendelea kujengwa na vibarua huenda ukaathiri muda muafaka wa kukamilika
kwa ujenzi wa soko hilo baada ya shughuli za ujenzi kusimama.
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Juma Idd, amesema kumekuwepo
kutoelewana kati ya mafundi/vibarua na mkandarasi kutokana na kuchelewesha
malipo.
Amesema kwa mujibu wa malalamiko ya vibarua pamoja na mafundi
dhidi ya mkandarasi huyo ni kuwa fedha zimecheleweshwa; fedha zinazokadiriwa
kuwa ni sh milioni 26 na hivyo kusababisha shughuli za ujenzi wa soko hilo
kusimama kwa zaidi ya siku nne sasa.
Taarifa za mgomo huo zilifika ofisi za Serikali ya Jiji la Mbeya
na kulazimika kufika katika eneo la soko na kuonana na mafundi hao.
Mkandarasi ametuma sh milioni 10 kwa ajili ya kupunguza deni kwa
vibarua na mafundi na kwamba fedha zilizosalia bado wanafanya mawsiliano na
mkandarasi.
Zoezi la kukabidhiwa soko lilikuwa lifanyike Oktoba 30 mwaka huu
lakini kutokana na hali ya mgogoro huo na mambo mengine ya siri zilizopo zoezi
hilo halitafanyika.
Imeelezwa kuwa soko hilo limekamilika kwa asilimia 75; vitu
ambavyo bado ni upakaji wa rangi wa baadhi ya sehemu za soko na kuweka vioo
katika baadhi ya sehemu za soko.
Vibarua
wanaofanya kazi katika soko hilo ni 129 na mafundi 29 ndiyo walio na mgogroro
na mkandarasi ambapo baadhi yao baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa soko hilo
waliamua kuacha kazi na kutoboa siri nzito za ubovu wa soko hilo Serikalini
lakini wakapuuzwa na kuambiwa kuwa hawana akili timamu
|
No comments:
Post a Comment