Vitu vilivyo tolewa na Katibu huyo ni pamoja na
Sabuni ,mafuta ya kupaka ,pedi ,miswaki,na dawa za meno ambavyo vyote
vinagharimu ya zaidi ya laki5.
Akikabidhi Msaada huo Mbuza amesema yeye binafsi
na kama kiongozi wa chama anapaswa kuhudumia makundi yote bila kujali itikadi
ya vyama wala dini hasa kwa kundi kama hilo la wafungwa ambao wanahitaji msaada
mkubwa hasa kwa mahitaji muhimu kama hayo yaliyo tolewa.
Amesema nivema kila mmoja katika shughuki zake
akajaribu kujiwekea utaratibu wa kutoa misaada kwa makundi mbalimbali
badala ya kuiachia jukumu hilo serikali pekee.
Kutokana na hali hiyo Mbuza amesema mara baada ya
kupatiwa nafasi hiyo ya uongozi ndani ya chama cha mapinduzi ambacho ndicho
chenye serikali atahakikisha anatumia fursa hiyo kuwatumikia wananchi wa
Jiji la Mbeya kwa moyo wake wote kama alivyo ahidi wakati akiomba kupatiwa
nafsi hiyo ndani ya Chama hicho cha CCM.
Aidha katika hatua nyingine Katibu huyo amewataka
wananchi wa Jiji hilo kuendelea kukipa nguvu chama cha mapinduzi ili kiendelee
kuwaletea wananchi wake maendeleo kwani katika kipindi hiki cha sasa asilimia
kubwa ya viongozi wa chama ngazi ya Wilaya na Mkoa imeshikiliwa na vijana wenye
nguvu na uwezo wa kuwatumikia wananchi wake.
Picha na Mbeya yetu Habari na Emanuel
Madafa,Mbeya
2 comments:
Big up Mbuza, usisahau kuchukua fomu ya Ubunge 2015, Yes You Can.
Bahati mbaya he is no longer with us, rip mtafutaji wa kweli
Post a Comment