CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya
ya Mbeya Mjini Kimepata vingozi wapya baada ya
kufanyika kwa uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi katika viwanja vya Sokoine
jijini hapa huku vijana na wanahabari wakig'ara katika nafasi mbalimbali.
Akitoa taarifa za uchaguzi huo Katibu
wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Raymond Mwangwala amesema uchaguzi huo
ulikwenda vizuri licha ya kutokea kwa kasoro chache.
Nafasi zilizo kuwa zikiwaniwa na
wagombea hao ni pamoja na nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
(Nec),Mwenyekiti wa Wilaya, nafasi ya wajumbe wawili wa Mkutano mkuu wa
Mkoa, Wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa Taifa na wajumbe 10 wa Halmashauri kuu
ya Wilaya.
Katibu huyo aliwataja wagombea
walioshinda katika nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni Ephraim Mwaitenda
aliyepata kura 552 baada ya kuwashinda wapinzani wake Japhet Mwasango
aliyepata kura 308 na Emily Mwaituka aliyeambulia kura 142.
Alimtaja aliyeshinda nafasi ya Unec
kuwa ni Sambwee Shitambala aliyepata kura 653 baada ya kuwaacha kwa mbali
wapinzani wake ambao ni Stephen Mwakajumilo aliyepata kura 278, Fatuma Kasuga
aliyeambulia kura 67 huku Daniel Fusi akijinyakulia kura 17.
Kwa upande wa nafasi ya wajumbe
wawili wa kuwakilisha mkutano mkuu wa Mkoa walioshinda ni Jackson Numbi
aliyepita kwa kura 513 na Tonebu Chaula aliyepata kura 485 baada ya kuwamwaga
wagombea wenzao wawili Israel Mwakasitu na Hollow Mayuma.
Na
Venance Matinya, msaidizi wa Kalulunga blog
|
No comments:
Post a Comment