Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, October 1, 2012

CCM MBEYA MJINI CHAPATA UONGOZI

 Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini  Raymond Mwangwala 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya  Mbeya  Mjini Kimepata vingozi wapya   baada ya kufanyika kwa uchaguzi  Mkuu uliofanyika juzi katika viwanja vya Sokoine jijini hapa huku vijana na wanahabari wakig'ara katika nafasi mbalimbali.

Akitoa taarifa za uchaguzi huo Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini  Raymond Mwangwala amesema uchaguzi huo ulikwenda   vizuri licha  ya kutokea kwa kasoro chache.

Nafasi zilizo kuwa zikiwaniwa na wagombea hao ni pamoja na nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa (Nec),Mwenyekiti wa Wilaya,  nafasi ya wajumbe wawili wa Mkutano mkuu wa Mkoa, Wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa Taifa na wajumbe 10 wa Halmashauri kuu ya Wilaya.

Katibu huyo aliwataja wagombea walioshinda katika nafasi ya Mwenyekiti  kuwa ni Ephraim Mwaitenda aliyepata kura 552  baada ya kuwashinda wapinzani wake Japhet Mwasango aliyepata kura 308 na Emily Mwaituka aliyeambulia kura 142.

Alimtaja aliyeshinda nafasi ya Unec kuwa ni Sambwee Shitambala aliyepata kura 653 baada ya kuwaacha kwa mbali wapinzani wake ambao ni Stephen Mwakajumilo aliyepata kura 278, Fatuma Kasuga aliyeambulia kura 67 huku Daniel Fusi akijinyakulia kura 17.

Kwa upande wa nafasi ya wajumbe wawili wa kuwakilisha mkutano mkuu wa Mkoa walioshinda ni Jackson Numbi aliyepita kwa kura 513 na Tonebu Chaula aliyepata kura 485 baada ya kuwamwaga wagombea wenzao wawili Israel Mwakasitu na Hollow Mayuma.

Na Venance Matinya, msaidizi wa Kalulunga blog

No comments: