|
Sura ya nje ya uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambao ni uwanja wa nyumbani wa Timu ya Prison inayoshiriki ligi kuu ukimilikiwa na Chama cha Mapinduzi umekuwa miongoni mwa miradi iliyotelekezwa katika ujenzi wa miundo mbinu yake hasa eneo la vyoo. |
|
Hii ni sehemu ya ndani ya uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambao umaarufu wake unajulikana tangu miaka ya themanini ambapo Tukuyu starz ilipandia daraja na kushiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka 1986 na kutwaa ubingwa mwaka huo huo, lakini kadiri miaka inavyoenda mbele huduma za uwanja zimekuwa zikirejea nyuma badala ya kuboreshwa |
|
Hiki ni miongoni mwa vyoo vinavyotumiwa na mashabiki wanaolipa kiingilio cha shilingi 3000 kwa mechi moja kwenye uwanja wa sokoine! Chama cha soka mkoa kinalalamika kuwa mahudhulio ya mashabiki ni kidogo hivi sasa katika uwanja huo, lakini kwa huduma hizi nani angependa kulipia huduma yenye viwango hivi? |
|
Hapa ndipo watumiaji walipofikia na kuendelea kupanga mizigo yao kuelekea nje baada ya choo kutokuwa na huduma zozote za usafi ! Idara ya afya ya halmashauri ya jiji imekuwa miongoni mwa taasisi za umma zinazolaumiwa na wadau wa soka kwa kufumbia macho hali hii |
|
Hiki ni moja ya vyoo vya pasport size kwenye uwanja wa sokoine ambavyo vinatumika kwenye michezo ya ligi kuu na shughuli mbalimbali za ujio wa viongozi kitaifa, uchaguzi mkuu wa chama na mikutano pamoja na matamasha mbalimbali! |
|
Kamera yetu imenasa mteja wa huduma za majengo haya zikiwa hazitosherezi na hasa milango yake ambayo upana wake haumwezeshi mtu kuingia kwa urahisi na badala yake kuingia kiubavu ubavu na matokeo yake watumiaji kuishia mlangoni na kumaliza shida zao |
|
Haya ndiyo mabafu ya uwanja wa sokoine jijini mbeya ambayo kwa sasa yamekuwa yakitumika kama vyoo na baadhi ya watumiaji kutokana na hali ya vyoo kuwa mbaya |
|
Ukuta wa duka la mojawapo lililo nje ya uwanja wa sokoine ukiwa unanyunyizwa kwa haja ndogo za watumiaji wake .
|
Hali ya uwanja wa sokoine jijini Mbeya imeelezwa kuwa mbaya na huenda ikawa chanzo cha magonjwa ya mlipuko katika jiji hilo wakati huu tukielekea kwenye msimu wa masika
1 comment:
Hii adha ya vyoo kwenye viwanja kama hiki ambavyo vimeendelea kung'ang'aniwa na CCM kwa mabavu, ilhali vilijengwa kwa nguvu ya umma, haitatatuliwa kutokana na ukweli kwamba CCM haina mkakati wowote wa kuzimudu gharama za kuboresha hivi viwanja zaidi ya kula tu mapato. Kihalali, viwanja hivi ni mali ya Wananchi na vilipaswa kuwa chini ya Manispaa.
Post a Comment