Na Esther Macha, Mbeya
Licha ya Mkoa wa Mbeya kuwa na idadi kubwa ya Mbwa bado imeonekana kuwa kuna tatizo kubwa kwa wafugaji kutokuwa na utamaduni wa kuchanja mbwa zao kwa madai kuwa grama za dawa za uchanjaji kuwa kubwa.
Akizungumza na Mwandishi wetu ofisini kwake , Ofisa Mifugo wa Mkoa wa Mbeya Dkt.Solomon Nong’ona alisema kuwa mbwa waliopo katika Mkoa ni wengi ukilinganisha na waliochangwa kwa Mkoa mzima.
Dkt. Nong’ona alisema kuwa Mkoa mzima una mbwa zaidi ya 70,000 lakini kati ya hao waliochanjwa ni wachache ukilinganisha na idadi iliyopo ya mbwa katika Mkoa.
“Kati ya julai 2011 mpaka julai 2012 ni mbwa 7,849 ambao ni sawa na asilimia 10 tu ya mbwa waliochinjwa hili ni tatizo kubwa hivyo kuna haja wafugaji wa mbwa wakaelimishwa si kutoa saababu za grama kubwa za uchanjaji”alisema.
Hata hivyo alisema Mbeya jiji pekee kwa wiki inakuwa na matukio 20 ya watu kuumwa na mbwa na kwamba wilaya ambazo zinaongoza ni pamoja na Mbeya Jiji ambapo watu 223 waliumwa na Mbwa, Mbozi 206,Chunya 64.
Aidha Ofisa Mifugo huyo alisema kuwa wafugaji wa Mbwa hawako makini na mifugo yao kwa kuona hakuna umuhimu wa kuchanja mbwa zao ambazo zinaleta athari kwa jamii.
Akizungumzia kuhusu grama za uchanjaji alisema kila mbwa anachanjwa kwa sh.5000 lakini badala yake wafugaji wa mbwa wamekuwa wakiona hiyo ni fedha nyingi na kuacha mifugo hiyo ikiendelea kuteketeza maisha ya wananchi wakati uwezo wa kuwachanja upo.
“Grama ambayo mimi naweza kuiona ni kwa mtu ambaye ameumwa na mbwa kwani Wilaya zingine hakuna hiyo dawa ambapo humlazimu mwananchi kupanda gari na kuja Mkoani kupata dawa hiyo kwa kutumia fedha ili aweze kufika hapa,ni jana tu alikuja mwananchi mmoja kutoka Ileje ambaye aliumwa na mbwa ”alisema.
Aidha alitoa wito kwa wafugaji wa mbwa kufuga mbwa na paka kwa ustaarabu ili zisiweze kuleta athari kwa jamii .
No comments:
Post a Comment