Na Bosco Nyambege,Ileje-Mbeya
Jumla ya wakazi 570 Wilayani Ileje Mkoani Mbeya wameunda kikundi kitakachoweza kujenga mitambo ya kufua umeme katika maporomoko ya mto Luswiswi katika Kijiji cha Bwenda yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati nane katika tarafa zaidi ya Bundali
Mitambo hiyo ni mradi wa umeme Luswisi kikundi cha mazingira Ileje mashariki ambao utaweza kusambaza katika kata 9 ambazo ni lwiswisi,Lubanda,Ngulilo,Sange,Ngulungulu,Kafule,Ikinga,Malangali na Ibaba.
Nia kuu ya kuanzisha mradi huo ni kuweza kuwasaidia wananchi wa kata hiyo ambao walikuwa wanatamani kupata nishati hiyo lakini hawakuweza kupata nikutokana na Tanesco kutowafikishia umeme wakazi hao kwa wakati muwafaka
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi huo Lukasi Mtafya mpaka sasa mradi huo unaendelea kuchunguzwa kwa kiwango kikubwa kwa kushirikiana na mradi wa nishati ya umeme vijijini (Rural energing Agency)kupitia Benki ya Dunia
Amesema kuwa katika hatua iliyofikiwa ni kupima kasi ya maji pamoja na usalama wa maji kwa matumizi ya binadamu
Hata hivyo Mtafya amesema kuwa kikundi kinatarajia kukusanya shilingi milioni36,Serikali inatarajia kuchangia kiasi cha shilingi miliono 146 na Halmashauri nya Wilaya ya Ileje inatarajia kuchangia kiasi chas shilingi milioni 38.
Mtafya amesema kuwa mradi huo utakapo kamilika wanatarajia kusambaza umeme huo katika sehemu mbalimbali za makazin ya watu pamoja na sekta mbali mbali za kiserikali
Kwa upande wa wananchi waliopata wasaa wa kuzungumzia suala hilo wamesema kuwa wanashukuru kwa wataalam hao kuweza kugungua maporomoko hayo kwani ni muda mwingi walikuwa wanatamani kupata umeme lakini ilikuwa wanpifgwa kalenda
Hivyo wameiomba serikali kuweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa wakati mfupi.
No comments:
Post a Comment