SAKATA la MKUU wa Wilaya ya Mbarali Gulamu Hussen Kiffu kunusurika kuumizwa na wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Chimala kilichopo Wilayani humo mkoani Mbeya baada ya kuvamia gari lake na kuvunja vioo,kutoa upepo wa matairi kutokana na Serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi, watu watano wamefikishwa mahakamani.
Kutokana na vurugu hizo zilizotokea chuoni hapo jana jioni, Jeshi la polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wanafunzi sita akiwemo Mkuu wa Chuo hicho Francis Mtega kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu zilizopelekea kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.
Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athuman alisema baada ya mkuu wa wilaya kuongozana na baadhi ya viongozi wa serikali hususani kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe ndipo hapo walipovamiwa na wanachuo hao.
Alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kuwasili Chuoni hapo kwa lengo la kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya wanafunzi walivamia gari la Mkuu wa Wilaya na kuanza kuvunja vioo kwa kutumia mawena kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.
Kamanda Athumani alisema tukio hilo linaonesha ni mpango uliokuwa umepangwa na uongozi wa Chuo kwa muda mrefu kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania na lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe ili kitambulike na Serikali na kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini.
Aliongeza kuwa kitu cha kushangaza ni madaraka aliyonayo mkuu wa chuo hicho ambapo yeye mwenyewe ni mwalimu na mhasibu na kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali kilikuwa ni kitu cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo.
Alisema katika uchunguzi wa awali umebaini kuwa chuo hicho kimeanza muda mrefu na tayari kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali bila ya serikali kutambua kama hakijasajiliwa na hakitambuliki.
Kwa hisani ya Venance Matinya, Mbeya.
1 comment:
Mpaka chuo kinatoa wahitimu, wahusika/serikali ilikuwa wapi? viongozi wa mitaa, kata, wilaya, tarafa na wilaya walikuwa wapi?
Watu wanafanya mizaha hadi kwenye fani ya afya. Ni hatari sana. Kweli ccm imechoka.
Post a Comment