Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 17, 2012

WATANO WAFA MBEYA AKIWEMO MAMA NA NA WATOTO WAKE WAWILI


WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la familia ya mama na watoto wake wawili waliofariki kufuatia ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao wakiwa wamelala.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya  mrakibu mwandamizi Barakiel Masaki, tukio hilo lilitokea  Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 4:55 usiku.

Alisema wanafamilia hao wakiwa wamelala nyumba yao ilianza kuwaka moto na kwamba walipoteza maisha kutokana na kukosa hewa kufuatia moshi mzito ulioenea ndani ya nyumba.

Amewataja wanafamilia hao waliokufa ni mama mzazi  Upendo Paul(24) na watoto wake ambao ni Tecra Paul (4) na Aman Paul wote wakazi  wa Ilemi darajani jijini Mbeya.

Masaki alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa bado hakijajulikana na miili ya maremu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoani hapa.

Aidha  ametoa wito kwa  wananchi kuchukua tahadhari kutokana na majanga ya moto  yanayotokea  mkoani  hapa.

Wakati huo huo mkazi wa majengo Mkwajuni  wilayani  Chunya Sprian Majiyashamba(58) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuumua mke wake kwa kumchoma kisu   kutokana  ugomvi wa kifamilia.

Kaimu kamanda Masaki  amesema marehemu  alifahamika kwa  jina la Secilia Dotabarabara(64) ambaye alichomwa kisu na mume wake kwenye titi la kushoto na kusababisha kifo chake  papo hapo.

Masaki  amesema kuwatukio hilo lilitokea Agosti 16 mwaka 2012 majira ya saa 4:00 katika kijiji cha majengo  wilayani chunya na kutaja chanzo cha kifo hicho kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

Katika tukio lingine mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha  nyakazobe wilayani Mbarali amemuua mume wake kwa kumpiga  na kitu kitu kizito kichwani kutokana kutokana na na ugomvi wa kifamilia.

Akielezea tukio hili  Masaki  amesema limetokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku kijijini hapo,na kwamba Christina Msiyunga(24) alimuua mume wake Geoge Lova(26) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Amesema   mtuhumiwa  wa tukio hilio amekamtwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika,aidha aliwaomba wananchi  kutatua migogoro kwa amani ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima.

Kwa hisani ya Joachim Nyambo

No comments: