Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 1, 2012

MZIMU WA KUTOJUA KUSOMA WATIKISA


na Christopher Nyenyembe, Mbeya
MZIMU wa kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu bado unaendelea kuwaumbua wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 na kufaulu kuingia kidato cha kwanza wapatao 105.
Tatizo hilo limeibuka Wilaya ya Mbeya kutokana na ukaguzi wa ndani unaondelea kufanywa na viongozi wa shule walikopelekwa wanafunzi hao, maofisa elimu kupita katika shule na kubaini wanafunzi hao.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa msaada wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umebaini idadi kubwa ya wanafunzi katika Wilaya ya Mbeya ambao hawajui kusoma na kuandika walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wafaulu.
Akizungumzia tatizo hilo, Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mbeya, Magret Mbwilo, alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema uchunguzi wa kina unaendelea, ili kujua taarifa za wanafunzi hao kutoka kwenye shule walikuwa wakisoma na kujua alama zao tangu awali.
Akizungumzia kuhusu wanafunzi hao kuendelea na masomo wakati hawajui kusoma na kuandika, alisema baada ya kutoka kwa matokeo ya darasa la saba, wizara iliagiza mikoa na wilaya kufanya uchunguzi katika shule mbalimbali, ili kubaini watoto ambao wamefaulu lakini hawajui kusoma na kuandika.
Hata hivyo, alisema kutokana na hali hiyo wao hawawezi kusema lini watafanya maamuzi, kwani wanasubiri tamko la wizara juu ya watoto hao.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments: